25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa azitaka benki kupitia riba

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amezitaka benki nchini zipitie upya riba zao ili Watanzania waweze kukopa na kurejesha kwa urahisi.

Alisema riba kubwa zinazotozwa na baadhi ya benki, huduma zisizokidhi mahitaji na uelewa mdogo wa masuala ya kifedha, ni miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo wananchi wanapotaka huduma za kifedha.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana alipokuwa akifungua mkutano wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi (COBAT) uliofanyika mjini hapa.

Mkutano huo ulijumuisha wajumbe kutoka mikoa 10 ya Kigoma, Lindi, Simiyu, Manyara, Katavi, Mbeya, Mwanza, Morogoro, Singida na Dodoma kati ya mikoa 18 ya Tanzania Bara ambayo bado haina benki za wananchi ila ipo katika hatua za kuanzisha.

Alisema changamoto nyingine ni kutokuwepo kwa taarifa mbalimbali za sheria na taratibu ambazo zinakwamisha ufanisi wa kiutendaji kwa baadhi ya taasisi, hasa zile zinazolenga kuwahudumia watu wa kipato cha chini.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles