33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa awakaribisha wawekezaji kutoka Rwanda

Mwandishi Wetu

Waziri MKuu Kassim Majaliwa, amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Rwanda kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali na Serikali itawapa ushirikiano wa kutosha.

Ameyasema hayo leo Juni 11, alipokutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Rwanda, Donatille Mukabalisa, ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma.

Amesema Serikali ipo tayari kuwapokea wawekezaji kutoka katika nchi hiyo ili waje kuwekeza katika sekta mbalimbali zikiwemo za viwanda, kilimo, madini na utalii, Tanzania na Rwanda ni nchi zenye uhusiano mzuri, hivyo amemwakikishia Spika Donatille kwamba Serikali itauimarisha uhusiano huo.

“Serikali inatekeleza mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) ambao utarajiwa kusaidia katika usafirishaji wa mizigo kwenda hadi nchini Rwanda,” amesema Waziri Mkuu.

Kwa Upande wakeSpika Donatille ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa inaoutoa kwa Serikali ya Rwanda, hivyo amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba watauendeleza.

Spika huyo amesema ushirikiano wa Tanzania na Rwanda ni muhimu katika uchumi kwa kuwa wanatumia bandari ya Dar es Salaam katika kusafirisha asilimia kubwa ya mizigo yao, hivyo wananchi nao wanatakiwa wawe na ushirikiano katika nyanja mbalimbali kama za kibiashara.

Aidha Spika huyo ametumia fursa hiyo kuwakaribisha Watanzania wakawekeze nchini Rwanda. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles