24.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

MAJALIWA AONYA MATAMKO YA MAWAZIRI

Na MWANDISHI WETU -DODOMA

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka mawaziri na naibu mawaziri wao wajiepushe kutoa matamshi yasiyotekelezeka  kuepuka mkanganyiko serikalini.

Kauli hiyo aliitoa jana wakati akifungua kikao kazi cha mawaziri kwenye ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma.

Alisema ni vema  viongozi hao kabla ya kutoa matamko wakajiridhisha iwapo jambo hilo halitaleta athari za bajeti na  sera na kama lipo katika bajeti za wizara zao.

Pia amewataka viongozi hao wafanye kazi kwa kuzingatia maadili ya uongozi  kuithibitishia jamii kuwa Rais Dk. John Magufuli   aliwateua kutokana na uadilifu na uwezo wao katika utendaji.

“Tunao wajibu mkubwa kuhakikisha   kila mmoja wetu anafanya kazi kwa nguvu na bidii   kutimiza matarajio ya Rais Dk. Magufuli na wananchi wote kwa ujumla,” alisema

Aliwataka viongozi hao wajiwekee utaratibu wa kusikiliza hoja na shida za wabunge na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni.

Pia amewataka wafuatilie  na  kufanya tathmini ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo inayohusu sekta zao kwa kuwa wao ni wasimamizi wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali.

Waziri Mkuu amesema mawaziri na naibu mawaziri wanatakiwa wasimamie utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa kuanzia mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021.

Pia wasimamie utekelezaji wa ahadi zote zilizopo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015  na ahadi alizozitoa Rais Dk. Magufuli,  wakati wa kampeni za uchaguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles