23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa aishukuru Finland kuisadia Tanzania kuondokana na umasikini

Anna Potinus

Waziri mkuu Kassim Majaliwa, ameishukuru serikali ya Finland kwa jitihada ambazo nchi hiyo inazifanya kuisadia Tanzania kuondokana na umasikini ambapo amesema kuwa bado nchi ina fursa za uwekezaji na kwamba Serikali inaendelea kutengeneza mazingira rafiki na bora kwa uwekezaji.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi, Mei 23, ofisini kwake bungeni jijini Dodoma alipokutana na Balozi wa Finland hapa nchini
Pekka Hukka anayemaliza muda wake ambapo amesema kuwa Sekta ambazo makampuni ya Finland inaweza kuwekeza hapa nchini ni pamoja na TEHAMA, nishati, usafiri, uchakataji wa mazao ya kilimo na misitu.

“Tunaishukuru Serikali ya Finland kwa misaada ambayo imeendelea kuitoa kama njia ya kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania za kuondoa umaskini pamoja na kuongeza makusanyo ya mapato ili kukuza uchumi wa nchi yetu,” amesema.

Aidha amemtakia heri Balozi Hukka ambaye anatarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa mwezi huu kwenda Tunisia ambako ndiko kutakuwa na kituo chake kipya cha kazi.

Kwa upande wake, Balozi Hukka amesema ataondoka Tanzania akiwa na kumbukumbu nzuri ambazo atazienzi na anataraji kukutana na Watanzania wengine ili aendelee kukuza mahusiano yaliyokuwepo.

Amesema Serikali za Tanzania na Finland zilisaini mkataba wa programu iitwayo Forestry and Value Chain Programme (FORVAC) ambao unalenga kuongeza faida za kiuchumi na kijamii kwa kupitia sekta ya misitu pamoja na kupunguza ukataji wa miti.

“Malengo hayo yatafikiwa kwa kukuza mnyororo wa thamani kwenye sekta ya misitu pamoja na kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji, sheria na sera katika sekta ya misitu,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles