24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa afuta umiliki mashamba 11 Ngara

k.majaliwaNa Mwandishi Wetu, Ngara

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameagiza kufutwa mara moja umiliki wa mashamba makubwa 11 yenye ukubwa wa ekari 7,700  katika   vijiji vya Kasharazi na Rwakalemera wilayani Ngara mkoani Kagera.

Mashamba hayo  hayana hati na yametelekezwa.

Alitoa agizo hilo jana  alipozungumza na wakazi wa vijiji vya Kasulo na Rwakalemera katika Kata ya Kasulo wilayani Ngara akiwa njiani kuelekea mkoa wa Geita.

Waziri Mkuu alilazimika kufanya mkutano huo mapema asubuhi baada ya kuitisha uongozi wa Wilaya ya Ngara ufike kwenye mkutano huo   kujibu kero za wananchi waliosimamisha msafara wake   wakati akielekea mjini Ngara.

Uamuzi huo ulitokana na hatua ya Waziri Mkuu kumwita kwenye mkutano huo, Ofisa Ardhi na Maliasili wa Wilaya, Betty Munuo   aeleze chanzo cha mgogoro wa ardhi katika vijiji hivyo.

Munuo ambaye amehamishiwa wilaya hiyo Agosti mwaka jana,  alisema aliyakuta malalamiko hayo na amefanya uchambuzi wa majina ya wamiliki wote wa mashamba na ilikuwa imepangwa wapatiwe notisi   wajieleze.

Katika orodha yake, Munuo alitaja wamiliki 18 wa mashamba makubwa lakini kati yao ni wamiliki saba tu ambao mashamba yao yana hati na matatu ndiyo yameendelezwa wakati manne hayajaendelezwa.

Akitangaza uamuzi wake, Waziri Mkuu aliwataja wamiliki wa mashamba yasiyo na hati kuwa ni pamoja na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Utumishi katika serikali ya awamu ya tatu, Joseph Rugumyamheto mwenye shamba na. 527 lenye ekari 505 lililopo Rwakalemera.

Waziri Mkuu aliagiza ifanyike sensa  kubaini kama wamiliki wa mashamba hayo yote ni Watanzania au la.

“Haya yenye hati nataka yafanyike mapitio ya hati zao na kubainisha ni namna gani walipatiwa hati hizo.

‘Nataka taarifa inifikie ofisini kwangu Dar es Salaam ifikapo    Machi 20, 2016,” alisema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles