24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mahiga: Tanzania inafuata mgawanyo wa madaraka vizuri tofauti na wengine

Mwandishi wetu, Mbeya

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk Augustine Mahiga,   amesema Tanzania ina mgawanyo wa madaraka na unaofuatwa vizuri tofauti na nchi nyingine.

 Akizungumza  juzi alipotembelea Ofisi za Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Mahiga  alisema ametembea nchi mbalimbali na kujifunza kwamba Tanzania mgawanyo wa madaraka unafuatwa.

“Mgawanyo wa madaraka  kwa mihimili ya dola ambayo ni  Serikali, Bunge na Mahakama upo na unafuatwa vizuri kulinganisha na nchi nyingine ambapo hata kuonekana haionekani kabisa na kama ilikuwepo basi ilikufa,” alisema Mahiga. 

 Akizungumzia kazi inayofanywa Majaji ya kusikiliza mashauri ambapo kuna wakati wanalazimika kufanya kazi kwa zaidi ya saa 18 kwa siku, alisema anatambua mchango zinazowakabili.

Pamoja na pongezi hizo, aliwataka  majaji hao, kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na utendaji uliotukuka.

 Aliwashauri majaji kuwa na maadili ya ziada na kuufanya Mhimili wa Mahakama kutekeleza majukumu kwa viwango vya juu.

Mahiga alisema kupitia kuongezeka kwa watu na kukua kwa Sayansi na Teknolojia, nchi yetu imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali zinazosababisha watu kubuni njia nyingi za uhalifu.

 Alisema  changamoto hizo zinasababisha kuwa na uhaba wa majaji kitendo kinachowalazimu kuwa na makadirio ya kusikiliza  mashauri  mengi zaidi tofauti na mipango ya kitaasisi na  kila mmoja  kulazimika  kufanya kazi kwa muda mrefu.

Naye Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Dk John  Utamwa, alisema  mikakati ambayo imekuwa ikitumiwa na Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya katika kuhakikisha mashauri yanaamuliwa kwa wakati ni  uwepo wa  miongozo ya utoaji huduma.

Akitoa mfano wa miongozo hiyo alisema ni pamoja na kuhakikisha kabla ya siku 21 nakala za hukumu zinatakiwa kuwa tayari lakini Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya nakala za hukumu hutolewa ndani ya siku ambayo hukumu hutolewa.

Mahiga yupo katika ziara ya kikazi mkoani Mbeya,  ambapo ameambatana na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga ambao wanakagua magereza na kutambua changamoto zinazowakabili wafungwa na mahabusu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles