26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MAHARAMIA WATELEKEZA BOTI YA MAFUTA BANDARI DAR

Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA), imekamata boti moja iliyokuwa inatumika kubeba mafuta wizi kutoka kwenye bomba la mafuta katika Bahari ya Hindi.

Boti hiyo imetelekezwa na watu wasiojulikana baada kukurupushwa na walinzi wa doria bandarini hapo  na kufanikiwa kukimbia kwa kupiga mbizi baharini huku boti hiyo ikikutwa na mabomu na milipuko kadhaa.

Kutokana na hali hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari, Mhandisi Deusdedit Kakoko, ameiomba serikali kuipatia mamlaka hiyo vitendea kazi muhimu ili kukabiliana na vitendo vya uharamia wa bomba la mafuta katika bahari ya hindi.

“Tunaomba tupatiwe vitendea kazi kwa ajili ya kikosi chetu kinachofanya kazi kubwa ya kupambana na uhalifu wa aina mbalimbali bandarini hasa magari ili kukiwezesha kikosi hicho kufanya kazi yake kwa ufanisi,” alisema Kakoko.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, ameahidi kuipatia Bandari hiyo vitendea kazi ambavyo viko ndani ya uwezo wake kama Waziri ili kuongeza udhibiti wa eneo la maji ya bahari lenye bomba la mafuta.

“Vitendo vinavyofanywa na wahalifu hao vinakwamisha juhudi za Serikali za kuimarisha miundombinu yake na kusabisha hasara kwa wenye mafuta na kuikosesha Serikali mapato kutokana na vitendo hivyo vya kutoboa bomba na kuiba mafuta,” amsema Dk. Mpango.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles