31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama Kuu: DPP kuzuia dhamana ni kukiuka Katiba

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

MAHAKAMA Kuu imesema kifungu namba 148(4) kinachompa mamlaka Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuzuia dhamana kinakiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kinamfanya DPP awe hakimu ama jaji kwa kesi yake mwenyewe.

Hayo yalisemwa jana wakati wa kutoa  uamuzi wa jopo la majaji watatu, Jaji Kiongozi Shaabani Lila, Jaji Sekieli Kihio na Jaji John Ruhangisa kwenye kesi iliyofunguliwa na Jeremiah Ntobesya.

Ntobesya aliomba kifungu namba 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) kitangazwe kinakiuka Katiba, hususan ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kifungu hicho kinampa madaraka DPP kuweka hati mahakamani ya kupinga dhamana.

Ntobesya alidai kwa mujibu wa ibara hiyo ya Katiba, matumizi ya kifungu namba 148 yanakiuka haki ya msingi ya mtuhumiwa kusikilizwa na hivyo kukiuka Ibara ya 13(6)(b), inayosema mtu anaonekana hana hatia mpaka ithibitishwe vinginevyo.

Wakitoa uamuzi, jopo la majaji hao lilikubaliana na hoja ya mwombaji na kutangaza kifungu hicho kinakiuka Katiba, hususan Ibara ya 13(6)(a).

“Kwa mujibu wa namba 148, kinamfanya DPP awe hakimu ama jaji kwa kesi yake mwenyewe, kukiuka misingi ya haki ya kusikilizwa.

“Kifungu hiki kinamnyima mtuhumiwa haki ya kusikilizwa katika masuala ya dhamana na kumfanya awe kama mtu aliyetiwa hatiani.

“Kizuizi kama hiki cha dhamana kinaweka rehani haki ya mwananchi, kwa msingi huo mtuhumiwa akiwa chini ya polisi au akishtakiwa, lazima apewe nafasi ya kujitetea kabla haki yake haijavunjwa na DPP kupinga dhamana,” lilisema jopo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles