27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli awapa majukumu mazito Simbachawene, Bashe

Anna Potinus

Rais John Magufuli amewataka Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, George Simbachawene na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kufanya kazi kwa juhudi kwa kushirikiana Wizara nyingine na wananchi ili kuhakikisha wanaleta maendeleo ya kiuchumi

Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Julai 22, Ikulu Jijini Dar es salaam baada ya kuwaapisha viongozi hao ambapo amewataka kutekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa na kutosikiliza maneno ya watu bali wamtangulize Mungu mbele.

“Nendeni mkawasimamie wakulima wanyonge, mkafanye kazi zenu kwa kumtanguliza Mungu mbele kwani mtapigwa vita, mtazungumzwa lakini mengine muyavumile kwasababu Mungu ndiye ametaka muwe katika nafasi zenu, kashirikianeni na wanyonge nina uhakika mtafanya makubwa,” amesema.

Amegusia suala la muungano ambapo amemtaka Waziri Simbachawene kusimamia suala hilo na kuwa chachu ya kuunganisha muungano ambapo ameagiza kusimamia utoaji wa vibali vya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kwa wawekezaji na kuhakikisha hawacheleweshewi vibali hivyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, George Simbachawene

“Pasiwe na ucheleweshwaji wa kutoa vibali vya NEMC kwa viwanda vyetu, sisi tunataka kuwa na viwanda vya kutosha na wawekezaji wasiwekewe vipangamizi kwa visingizio vya NEMC, vibali hivi vitoke na ikiwezekana wawekeze kwanza vibali vitakuja baadae kwasababu vitu vyote hivi ni vyetu,” amesema.

Aidha amemtaka Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, kuhakikisha anaisimamia sekta hiyo ipasavyo ili wananchi waweze kupata utajiri kutokana na kilimo ambapo amemtaka kushugulika na wafanyabishara wanaodanganya wananchi.

“Ninakupongeza Hussein Bashe kwa kuchaguliwa kuwa Naibu Waziri wa sekta ambayo ni muhimu sana, nimekuwa nikikusikiliza bungeni michango yako imekuwa ni mizuri, umekuwa ukitoa ‘analysis’ ya namna gani kilimo kinaweza kikaleta faida katika uchumi wetu, sasa zile zilikuwa ni za bungeni ninataka ukaziweke kwenye vitendo ndio maana nimekuweka Wizara ya kilimo ili yale uliyokuwa ukiyazungumza bungeni na tukayafurahia sasa ukayafanyie kazi kwelikweli,” amesema.

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

“Ssa hivi kuna tatizo kule Kagera, tumewaambia watu wauze kahawa na wawekezaji kutoka nje wanaotaka kununua waje lakini wanunue kuanzia Sh. 1,500 na kuendelea kwasababu kuna michango inayotakiwa kulipwa kwenye halmashauri zetu na kwenye serikali, wafanyabishara wachache wameshaanza kudanganya wananchi kwamba fedha zimeshapelekwa kule za kulipia kahawa sasa wafanyabiasha wa namna hiyowanaodanganya wanachi wasiuze kahawa wao watazinunua ni lazima washughulikwe kwa mkono mmoja bila kuwaonea huruma,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles