24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli atumbua, ateua

Mwandishi Wetu

Rais John Magufuli, amefanya uteuzi, utenguzi na mabadiliko ya viongozi mbalimbali wakiwamo wakuu wa mikoa, wilaya, makatibu na naibu makatibu wakuu.

Katika uteuzi huo, Rais Magufuli pia ameteua mabalozi 12, akiwamo aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), Modestus Kipilimba, ambaye ameteuliwa kuwa Balozi ambapo kituo chake cha kazi kitatangazwa baadaye.

Uteuzi huo uliotangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi, John Kijazi leo Septemba 20, Rais Magufuli amemteua Lowata Sanare kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na kutengua uteuzi wa Kebwe Steven aliyekuwa mkuu wa mkoa huo na Musa Masele kuwa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro.

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Charles Kabeho, amehamishiwa Wilaya ya Chato na Mkuu wa Wilaya ya Chato Msafiri Mtemi amehamishiwa Wilaya ya Tarime.

“Rais Dk. Magufuli ameteua mabalozi 12 ambao wataiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali. Uteuzi huo unatokana na vituo hivyo ama kuwa wazi, mabalozi kumaliza muda wao, kustaafu au kurejeshwa nyumbani ambapo watapangiwa kazi nyingine,” amesema Kijazi.

Kijazi ameyataja majina ya mabalozi walioteuliwa ni Mohamed Mtonga, Dk. Jilly Maleko, Dk. Benson Bana, Meja Jenerali Mstaafu, Anselimu Bahati, Profesa Emmanuel Mbennah, Maimuna Tarishi, Meja Jenerali Mstaafu, Gaudence Milanzi, Ali Jabir Mwadini, Dk. Modestus Kipilimba, Jestas Nyamanga, Profesa, Dk. Kennedy Gaston na Mhandisi Aisha Amour.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles