27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli alivyojibu kero za wafungwa Butimba

Anna Potinus

Rais John Magufuli amewataka wafungwa na mahabusu kuwa wavumilivu na kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu ili awasamehe makosa yao ambapo ameahidi kufanyia kazi malalamiko yao yote na kumtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro, kushugulikia kesi ambazo hazina mshiko.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Julai 16, alipotembelea gereza la Butimba na kupata fursa ya kusikiliza kero wanazokutana nazo wafungwa na mahabusu hao ambapo amewataka maofisa wa polisi wa gereza hilo kutowaadhibu kwa kuuliza na kutoa maoni yao na kwamba iwapo watafanya hivyo wasijutie hatua atakazozichukua juu yao.

“Kufungwa au kuwa mahabusu haimaanishi kuwa hauna haki ya kupata utu wako ndio maana nimekuja hapa kuwasalimu, nimesikia changamoto zenu na za maaskari wangu nao wanafanya kazi katika mazingira magumu ninajua kuna waliofungwa ambao hawajafanya makosa na ninajua kuna waliokaa mahabusu wanacheleweshewa kesi zao ili wasipate kazi za au kwasababu hawajazungumza vizuri na polisi,” amesema.

“Mkuu wa magereza hawa watu wote waliotoa kero zao hapa wasisumbuliwe wala asitokee mtu akawauliza kwanini waliuliza swali na wakaanza kusulubiwa na ninataka niwaambie nitajua na nikijua msinilaumu kwa maagizo nitakayoyatoa, nimekuja kwa wapiga kura wangu na siku nyingine nitakuja tena,” amesema.

“Niliyoyaona yamenigusa mimi ni kiongozi wenu lakini pia ninamuogopa Mungu hivyo ninawaomba mvumilie na nimekuja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, RPC ambaye yeye ndiye msimamizi wa polisi wote katika Mkoa huu, kamati ya ulinzi na usalama, wanajeshi saa ninachowaahidi ni kwamba nimewasikia sasa mniache nikayafanyie kazi,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles