27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Magonjwa ya kitambi yanayowatesa wanawake

ubonge

TATIZO la kuvurugika kwa homoni linawakabili wanawake wengi ambao wamekuwa wakitumia kila mbinu ya kuliondoa bila mafanikio.

Miongoni mwa homoni hizo ni estrogen, progesterone, Follicle Stimulating, Luteinazing na Testotestorone.

Leo utajifunza jinsi gani unavyoweza kuangamiza matatizo ambayo hukuzaliwa nayo hasa yale yanayohusiana na hedhi yako.

Mambo yanayoashiria una tatizo katika homoni zako za kike

1. Kuwa na hedhi ya muda mrefu zaidi ya siku saba
2. Kuwa na hedhi yenye kuambatana na maumivu makali sana
3. Kuwa na hedhi yenye kuambatana na kichefuchefu, kuharisha
4. Kuwa na hedhi iliyojaa woga mkubwa sana
5. Kuwa na hedhi ambayo haina mpangilio, Unaweza kuingia mara tatu kwa mwezi, mara mbili au unaweza usipate kabisa hata miezi sita hadi mwaka.
6. Kuwa na ndevu nyingi kupita kiasi sehemu za usoni, kifuani
7. Kuwa na kitambi cha tumbo la chini (Abdominal obesity)
8. Kukosa mtoto kwa muda mrefu
9. Kukosa hamu ya tendo la ndoa lenye kuambatana na maumivu makali
10. Mwili kuuma sana hasa misuli bila sababu ya msingi, kuumwa sana na kichwa bila sababu ya msingi.

Kinamama wengi wamekuwa wakieleza jinsi walivyosumbuka kutatua tatizo hilo na ninaweza kuwaweka katika makundi yafuatayo.

  1. Kundi la kwanza ni wale ambao ndio tatizo, nimeanza kuwaandama na hivyo wanajaribu kutafuta njia nyepesi za kuondoa tatizo kabla hawajafikia zile njia ngumu za hospitali za kuliondoa tatizo.

Wanawake wengi huwa ni waoga sana wa kuuguza uzazi wao hasa pale inapotokea hajaolewa na hajapata mtoto hivyo ikitokea ana tatizo kama hilo wengi huwa wanakuwa makini kutojishirikisha na njia hatarishi.

Wengi huwa nawauliza umefanya juhudi gani kuondoa tatizo? Hunijibu ‘yaani mimi naogopa nimeambiwa inaweza kunipelekea kizazi kikaondoka’.

Si kweli afya yako ni hazina yako, wewe ndiye mwenye mamlaka wa kuruhusu tiba fulani itekelezeke au hapana.

  1. Kundi la pili ni wale watu ambao wametumia kila mbinu za kutatua matatizo kwa kuanzia ngazi za juu lakini hawajapata suluhisho.

Sasa anaanza kutafuta suluhisho kwa upande wa pili ili aone kama huko pia atafanikisha kuifikisha afya yake mahali stahiki. Hawa huwa wamesumbuka kwa wataalamu mbalimbali lakini hawajakata tamaa.

  1. Kundi la tatu ni wale watu waliotumia njia zote bila mafanikio hadi wametamkiwa na washauri wao hapo hutaweza kufikia malengo, shusha pumzi yako ipokee hali yako maisha yaendelee. Hawa ni watu ambao wanaishi katika msongo wa mawazo mkubwa sana.

Mwanamke huwezi kuwa na amani kama hedhi yako ina kasoro, kwani hiyo ndio nyota njema katika maisha yako kiafya, ni jukumu letu kuhakikisha inarudi katika misingi ya mwanzo na ufurahie hedhi yako.

Itaendelea wiki ijayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles