24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Magonjwa ya kitambi yanayowatesa wanawake

fatTUMEKUWA na makala mfululizo kuhusu magonjwa ya kitambi yanayowatesa wanawake na sababu za magonjwa hayo.

Wiki hii katika safu yetu tutaangalia mambo ya kufanya ili kupunguza vitu vinavyoongeza kiwango cha Insulin.

Ukitaka kuifanya insulin ifanye kazi ni kupunguza vitu vinavyoongeza kiwango cha insulin ndio maana wagonjwa wengi wenye PCOS wanapewa dawa kama Metformin (dawa za kuongeza utendaji kazi wa insulin).

Lakini hilo si suluhisho la kudumu katika maisha yako bali suluhisho pekee ni kuhakikisha vitu vinavyopandisha insulin vinaepukwa.

Jiko lako linaweza kuwa linakuuguza kabisa na ni wakati sasa wa kusafisha jiko lako na vyakula ambavyo uliambiwa ni adui yako kuanzia leo viwe rafiki yako.

Vyakula kama mahindi, mtama, ulezi, viazi, ngano na aina yoyote ya vinywaji vyenye sukari na pombe aina zote.

Kula vyakula kama samaki, karanga, ufuta, alizeti, korosho, almonds, nyama aina yoyote, mayai kwani ni vyakula safi kwako na tiba ndani ya muda mfupi.

Ugonjwa ni wa kurithi kwa asilimia ndogo
Ugonjwa huu wa PCOS ni ugonjwa wa lishe ambao hauzingatii kanuni na masharti ya tiba.

Tukiongelea lishe mbovu watu wengi wanajua ni ile hali ya kula vyakula vya mafuta, kula sana, kunywa pombe na kutofanya mazoezi.

Tafakari kwa kina vyakula ambavyo vinavuruga homoni za mwili wako na hatimaye kukuletea ugonjwa huu.

Nimeeleza kwa kina namna gani vyakula vya wanga vinavyotuletea ugonjwa wa PCOS na suluhisho lake.
Hivyo unapotaka kusema huu ugonjwa ni wa kurithi hakikisha umeondoa visababishi vingine vyote vya ugonjwa huo.

Huwa nasema kila siku huwezi kuniambia kwenu kuna watu wenye ndevu na wewe basi umerithi kutoka kwa bibi yako si kweli.

Madhara ya kuvurugika kwa homoni mwilini

Sayansi ya homoni “Endocrinology” naifananisha na vitabu 10 ambavyo nimevipanga kwa wima kwenye meza, ikitokea nimekisukuma kitabu kimoja kikaangukia kitabu cha pili hivyo vitabu vyote vitaanguka kwa kufuata mlolongo ule ule.

Hii namaanisha kwamba homoni moja ikitoka katika misingi yake homoni zingine pia zinavurugika kwa kiwango kikubwa sana na ndio maana watu wenye PCOS huwa wana dalili zaidi ya moja kwani ugonjwa huu unahusisha mvurugiko wa homoni nyingi.

Tiba ya ugonjwa huu ni lishe hata wewe unaweza kuanza leo kuhakikisha unasawazisha homoni zako zote zirudi katika misingi.

Zifuatazo ni baadhi ya homoni ambazo huvurugika mwilini na kusababisha mtu kupata PCOS.
Kiwango cha Estrogen huongezeka kupita kiasi. Hii inasababishwa na insulin kuisisimua ovari kufanya kazi kwa kiwango kikubwa na hii inapelekea kiwango cha homoni hii kuwa juu kwenye damu.

Madhara ya homoni hii kuwa katika kiwango kikubwa katika mwili inaweza kusababisha ukuta wa kizazi kujengeka na kuwa mnene kupita kiasi na hatimaye unaweza kuwa hatarini kupata saratani ya kizazi.

Na hii ndio sababu kubwa ya kupata hedhi nzito kupita kiasi yenye mabonge ya damu, kwa sababu kazi kubwa ya estrogen ni kukufanya  uonekane mwanamke na ndio homoni ambayo inajenga ukuta wa kizazi kila mwezi ili kama mimba ikitungwa mtoto aje ajishikize kwenye ukuta imara.

Lakini inapotokea kiwango chake ni kukubwa ukuta mnene utajengwa kila mwezi na inapokuwa mimba haijatungwa ukuta utabomolewa na kama ni mnene damu nyingi zitatoka.

Ukiona dalili hizo fika hospitali maana kuna hatari kubwa ya kuishiwa damu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles