24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Magavana na mpango wa siri kuondoa ukomo wa madaraka

ISIJI DOMINIC

MJADALA mkubwa unaoendelea nchini Kenya zikiwa zimebaki takribani miaka mitatu kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu ni kuwapo kwa Kura ya Maoni kubadilisha baadhi ya vipengele vya Katiba ambayo ilipitishwa mwaka 2010.

Kura ya Maoni itafanyika kutokana na swali au maswali yatakayoulizwa na hadi sasa haijajulikana ni aina gani ya swali ambalo limedhamiriwa kuulizwa. Wanaopinga kufanyika kwa kura ya maoni kubadilisha Katiba wanadai fedha nyingi zitatumika huku wale wanaounga wanadai bora zitumike fedha nyingi lakini ikapatikana Katiba bora zaidi ambayo itahakikisha hakuna ghasia kila uchaguzi mkuu unapofanyika.

Chama tawala cha Jubilee na Muungano wa vyama vya upinzani, NASA, wote wanakubaliana kwamba endapo kura za maoni zitafanyika basi iwe ni kwa manufaa ya wananchi na kuimarisha demokrasia badala ya kutengeneza vyeo kwa baadhi ya viongozi walioshindwa kwenye uchaguzi.

Huku Wakenya wakisubiri swali au maswali yatakayoulizwa kuhalalisha Kura ya Maoni, kamati maalumu ya Baraza la Magavana wameandaA nyaraka inayopendekeza kuondolewa kwa muhula miwili ya uongozi.

Hii ni kinyume na Katiba Ibara 180(7) inayomzuia gavana au naibu gavana kuhudumu kwa zaidi ya mihula miwili. Hoja inayotolewa na Baraza la Magavana ni kwamba si haki wao kuwekewa ukomo wa kukaa madarakani kwa mihula miwili wakati wabunge na wajumbe wa mabaraza ya wawakilishi wanaruhusiwa kugombea kila kunapofanyika uchaguzi.

Kigezo kilichotumika kuweka ukomo wa madaraka hususani kwa magavana ni kuwalinda wananchi kwa viongozi wenye uchu wa madaraka. Ni dhahiri kama ukomo usingekuwapo magavana wanao uwezo wa kutumia rasilimali walizonazo kuhakikisha hawaondolewi madarakani tofauti na wabunge au wajumbe wa mabaraza la wawakilishi ambao hawana ushawishi mkubwa kuchochea uchaguzi.

Huenda hoja ya kamati maalumu ya Baraza la Magavana kutaka kuondolewa ukomo wa uongozi inatokana na mpango wa Kura za Maoni kubadilisha Katiba itakayoruhusu kurudishwa kwa nafasi ya waziri mkuu na naibu waziri mkuu wawili huku baadhi ya viongozi wakitaka Rais Uhuru Kenyatta awanie nafasi ya Waziri Mkuu muhula wake wa pili ukimalizika.

Japo Mwenyekiti wa Baraza la Magavana, Wycliffe Oparanya, amesema hajapokea ripoti hiyo amesisitiza itakapowasilishwa ataitisha kikao cha magavana ili watoke na kauli moja. Oparanya ni mmoja wa wajumbe wa kamati maalumu ya baraza hilo chini ya wenyeviti wenza Profesa Kivutha Kibwana wa Makueni na Kiraitu Murungi wa Meru ambao tangu kuanzishwa walikutana mara moja tu Oktoba mwaka jana na hivi karibuni watakutana tena.

Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Joyce Laboso (Bomet), Anyang’ Nyong’o (Kisumu), Amason Kingi (Kilifi), Charity Ngilu (Kitui), Francis Kimemia (Nyandarua), Paul Chepkwony (Kericho), Ali Roba (Mandera) na Cornel Rasanga (Siaya).

Mara tu kamati hii ya watu 11 itakapomaliza kuandaa mapendekezo yake itawasilisha kwa kamati iliyoundwa na Rais Uhuru na kinara wa upinzani Raila Odinga na kupachikwa jina la Building Bridges.

Gavana wa Uasin Gishu, Jackson Mandago, ameweka wazi msimamo wake kupinga kuondolewa ukomo wa uongozi wa magavana akisema hata kama kiongozi alishindwa kutimiza ahadi yake ndani ya miaka kumi hataweza kuzitimiza akiongezwa miaka nyingine kumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles