26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Magaidi wapoteza ngome ya mwisho

BAGHOUZ, SYRIA

MAJESHI yanayoungwa mkono na serikali ya Marekani, jana yalitangaza kuwa yamelikomboa eneo la mwisho ambalo lililikuwa linadhibitiwa na wapiganaji wa kundi kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu, IS. Eneo ambalo limekombolewa na majeshi hayo kutoika kwa magaidi ni kijiji cha Baghouz kilichopo mashariki mwa Syria.

Taarifa iliyoripotiwa na mtandao wa Al Jazeera imesema kuwa majeshi hayo yanasaidiwa na Marekani yametangaza mwisho wa kundi hilo la kigaidi ambalo hapo awali lilijitangazia mamlaka ya kutawala eneo hilo.

Kukombolewa kwa kijiji cha Baghouz kunaashiria mwisho wa utawala wa magaidi wanaojiita Dola la Kiislamu. Awali magaidi hao waliyadhibiti maeneo makubwa katika nchi za Irak na Syria.

Katika harakati za kuyakomboa maeneo hayo zilizoendezeshwa na Marekani na washirika wake kwa muda wa miaka mitano magaidi wengi na raia waliuawa.

Rais Donald Trump jana alitangaza kwamba magaidi wa IS hawadhibiti tena sehemu yoyote nchini Syria. Hata hivyo, zipo taarifa kwamba milio ya risasi iliendelea kusikika kwenye maeneo yaliyokuwa yakikaliwa na magaidi hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles