25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Maelfu ya raia DRC wakimbilia Uganda

KAMPALA, UGANDA

MAELFU ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wamelazimika kukimbilia katika nchi jirani ya Uganda kufuatia machafuko yaliyozuka hivi karibuni katika nchi yao hasa katika mkoa wa Ituri.

Duru za habari zinaripoti kwamba, zaidi ya raia 400,000 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamekimbilia katika maeneo mengine ya nchi hiyo katika majuma ya hivi karibuni baada ya kuzuka machafuko katika mkoa wa Ituri.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, wengi wa wakimbizi hao wanajaribu kuvuka mpaka na kuingia katika nchi jirani ya Uganda.

Ripoti zinasema kuwa, raia nusu milioni wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamebaki bila makazi na wengine 400 wakiuawa kufuatia machafuko ya mwezi huu wa Juni pekee.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemorasia ya Congo anatarajiwa kuutembelea mkoa wa Ituri ambao kwa sasa unakabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu.

Mashirika mbalimbali ya kieneo na kimataifa ya misaada ya kibinadamu yametahadharisha kuhusiana na hali mbaya ya kibinadamu inayoshuhudiwa katika mkoa wa Ituri.

Ni miaka ishirini imepita sasa ambapo maeneo ya Mashariki na Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yanashuhudia hali ya mchafukoge na ukosefu wa amani, hali ambayo imewasababisha matatizo mengi wakazi wa maeneo hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles