30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MADRID  HAWAJAWAHI KUMUHESHIMU MESSI

ADAM MKWEPU NA MITANDAO


HAKUNA siku mshambuliaji wa  timu ya Barcelona, Lionel Messi  atasimama mbele ya mashabiki wa Real Madrid na kupewa heshima, si kwake wala watangulizi wake.


Ungeweza kuzungumza  kitu fulani baada ya tukio la Messi kuvua flana yake na kuitundika mbele ya mashabiki wa Madrid wakati amabo mabao yake mawili tayari yalishaamua nani mshindi katika mchezo dhidi ya mahasiimu hao wa Madrid.


Messi alikuwa katika kilele cha furaha hasa baada ya kutimiza mabao 500 tangu acheze mpira akiwa Barcelona pia kuwa  kinara wa mabao katika mchezo dhidi ya wapinzani wake hao akifunga jumla ya mabao 15 akiyapita yale 14 yaliyowekwa na Afredo de Stafano.


Mashabiki wengi wa Madrid hawakuchukizwa na kitendo cha Messi kutundika jezi bali bao walilofungwa muda wa lala salama tena na hasimu wao namba moja.


Kwa Madrid walijikuta wakiishiwa nguvu na kuona kipigo hicho ndio mwisho wa ubabe wao wakati ambao walikuwa wakisubiri miujiza zaidi itokee ili kushinda mchezo huo.


Kilichofanywa na Messi wiki iliyopita, kiliwahi kufanywa na Ronaldinho  mwaka 2005  baada ya kufanya vizuri katika mchezo wao dhidi ya Madrid katika Uwanja wa Bernabeu, lakini aliishia kuzomewa na mashabiki wa Madrid.


Mwaka 1983,  Diego Maradona akiwa mchezaji wa Barcelona aliwahi kushangiliwa kwa wingi na mashabiki wa Madrid.Swali kwanini isiwe kwa  Messi.


Labda kwa kuwa amewaumiza sana mashabiki wa Madrid, kwani Clasico yake ya kwanza Uwanja wa Nou Camp Messi alishinda mabao matatu wakati ambao timu yake ikishinda, Messi alifanya hivyo ata katika sare ya mabao 3-3.


Hata kama Madrid watashinda Ubingwa wa Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’ Messi amekuwa mwiba mchungu kwao katika michuano mingi ikiwamo ya La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya, pamoja na Kombe la Mfalme.


Mashabiki wengi wa Madrid walisikika wakimdhihaki  Messi kutokana na kitendo chake cha kutundika jezi yake kuwa  ni ukosefu wa akili ‘mtu mwenyewe hawezi ata kuzungumza vizuri,’ alisikia mmoja kati ya mashabiki waliokuwepo upande huo huku wingine akiimba  ‘Messi…Messi….ni nusu  ya binadamu aliyekamilika ’.


Wapo mashabiki wengine waliokuwa wakiimba kwa kumkebehi nyota huyo mwenye tuzo tazo za Ballon d'Or, hata hivyo jambo hilo lilionekana kuwa la kawaida kutokana na hisia za mashabiki hao baada ya timu yao  kufungwa katika mchezo huo.


Ni kawaida jambo kama hilo kutokea kwa Cristiano Ronaldo katika Uwanja wa Nou Camp kutokana na uhasama uliopo kati yake na Messi katika  miaka ya hivi karibuni.


Mashabiki wa Madrid siku zote uonesha upendo kwa kukipigania cha kwao huku wakionesha kuchukizwa na kile ambacho hawakipendi kutoka kwa wapinzania wao hao.


 Kiujumla mchezo kati ya Barcelona na Real Madrid ulikuwa na uhasama mkubwa wakati ambao Jose Mourinho alimfanya Messi kuonekana adui namba moja hadi sasa.


Miongozi mwa mchezo ulikuwa ule wa mwaka Aprili 2011 uliochezwa Uwanja wa Bernabeu ambapo Messi akiwa katika harakati za kuufukuzia mpiara na kuukosa na baadae kuulusha kwa mashabiki  kutokana na kukasilika.


Kitendo hicho kiliwaumiza sana mashabiki hao baada ya mchezo huo kumalizika kwa kutoka sare ya bao 1-1.
Siku chache baadae Madrid waliwafunga Barcelona katika fainalia ya Kombe la Mfalme katika Uwanja wa Mestalla.


Lakini wiki moja nyuma kabla ya mchezo huo beki wa Madrid alitolewa nje ya Uwanja na Messi alishinda mabao mawili wakati huo kipa akiwa Iker Casillas na Barcelona kufuzu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Kabla ya mchezo wa wiki iyopita, mashabiki wa Madrid hawakuzani kama Messi angefunga katika mchezo huo kutokana na kushindwa kufunga katika michezo sita kutofunga dhidi Madrid.


Lakini mashabiki hao walitakiwa kufaham zaidi ya wanavyoandika kuhusu nyota huyo ambaye ana kila rekodi katika mchezo wa soka Duniani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles