25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

MADIWANI WATISHIA KUWA ‘MABUBU’

Na MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM

BAADHI ya madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni wametishia kutozungumza katika vikao vya Baraza la Madiwani kwa sababu hoja zao hazifanyiwi kazi.

 

Tishio hilo walilitoa jana katika Kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi kujadili taarifa ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2017/18. Katika kikao hicho kila diwani aliwasilisha taarifa ya kata yake.

 

Madiwani waliotoa tishio hilo ni wa Kata ya Kigamboni, Doto Msawa (CCM) na Celestin Maufi wa Kata ya Mji mwema (Chadema).

 

“Mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Kigamboni umekuwa ukitengewa bajeti kila mwaka lakini haijengwi, sasa leo (jana) nazungumza kwa mara ya mwisho hapa,” alisema Msawa.

 

Aliitaja mradi mwingine wa ujenzi wa mfereji wa maji maeneo ya kituo cha polisi na mahakama ambavyo wakati wa mvua hufungwa kwa sababu ya kujaa maji.

 

Kwa upande wake Maufi, alisema taarifa ya ukarabati wa madarasa katika Shule za Sekondari za Kidete na Kibugumo imekuwa ikirudiwa rudiwa kila mara lakini hakuna utekelezaji unaofanyika.

 

“Tuna – copy na ku – paste hii taarifa, sasa na mimi itakuwa mara ya mwisho kuliongelea hili suala,” alisema Maufi.

 

Akizungumza katika kikao hicho, Meya wa Manispaa ya Kigamboni, Maabadi Hoja (CCM), aliwasihi madiwani hao wasisuse kwa sababu wao ni wawakilishi wa wananchi.

“Sipendi kusikia kauli kama hizi, mnawakilisha wananchi msisuse mtakuwa mnakosea, endeleeni kupambana na sisi tuko nyuma yenu kuhakikisha yanatekelezwa,” alisema Hoja.

 

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Stephen Katemba, aliahidi kuwa zabuni za miradi ya maendeleo zitaanza kutangazwa mwezi huu na kwamba miradi ya sekta ya elimu itapewa kipaumbele.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles