24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Madiwani Maswa: Busara itumike ugawaji vitambulisho vya Wajasiriamali

SAMWEL MWANGA-MASWA

Madiwani katika wilaya ya Maswa mkoani Simiyu wamewataka watumishi wa serikali waliopewa jukumu la kugawa vitambulisho vya wajasiriamali wilayani humo vililivyotolewa na Rais Dk John Magufuli kutumia busara na siyo nguvu na kutishia kufungia biashara zao.

Wakizungumza katika kikao cha baraza hilo kilichofanyika mjini Maswa wamesema kuwa wanasikitishwa na vitendo vya baadhi ya watumishi hao wa serikali kuwalazimisha kuchukua vitambulisho hivyo kwa kutumia nguvu na kutishia kuzifunga biashara zao jambo ambalo ni kinyume na maagizo yaliyotolewa na Rais Magufuli.

Wamesema kitendo cha kuwatumia askari polisi wenye silaha za moto katika kugawa vitambulisho hivyo na kuwakamata wafanyabiashara wanaodaiwa kutokuwa na vitambulisho hivyo kimezua sintofahamu na kuwafanya baadhi yao kuzikimbia nyumba zao kwa kuogopa kukamatwa na polisi.

“Haiwezekani mfanyabiashara ambaye ana duka la kuuza vitambaa vya nguo ambaye pia ana cherehani mbili hapa dukani na analipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania pia anatakiwa alipie tena vitambulisho vya mjasiriamali kwa sababu ana cherahani hilo suala ni unyanyasaji wa hali ya juu na halikubaliki,” amesema diwani wa Kataya Zanzui(CCM) Jeremiah Shigala.

“Kuna siku ya jumapili hapa Maswa mjini ilikuwa ni kamatakamata yaani watendaji wa Kata walikuwa wakiingia kwenye maduka ya kuuza vitambaa vya nguo na nguzo zilizoshonwa na kuwataka mafundi wote wa nguo kuchukua vitambulisho vya wajasiriamali na ukishindwa wanakueleza uache kushona huku wakitishia kuchukua kichwa cha cherahani,” amesema diwani wa viti maalum(Chadema) Frola Msuka.

Katika kikao hicho madiwani hao wamesema kuwa ni vizuri elimu ikatolewa kuliko kutumia nguvu katika zoezi hilo kwani walimsikilia vizuri Rais Magufuli wakati akikabidhi vitambulisho hivyo kwa Wakuu wa Mikoa kuwa waliokuwa wanalipa mapato yao TRA wasipatiwe vitambulisho hivyo vya wajasiriamali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles