28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Madiwani CCM Iringa watangaza kumng’oa meya, yeye adai bado ni meya

Fransic Godwin -Iringa

MADIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Manispaa ya  Iringa, wamemuondoa meya halmashauri hiyo, Alex  Kimbe, kupitia  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kura za kutokuwa na imani naye 14 kati ya 26 .

Kikao hicho cha kumuodoa kilifanyika chini ya ulinzi mkali wa  polisi ambapo wajumbe  walikuwa wakiingia kwa  barua maalumu ya mwaliko.

Mwenyekiti wa kikao  hicho Joseph Ryata  ambae ni Naibu Meya akitangaza matokeo ya  kura, alisema kura zilizopigwa ni 26 ambapo 12 ziliharibika na  14  zilimtaka Kimbe  kuondolewa katika nafasi yake .

“Ndugu wajumbe zoezi letu la mchakato wa kupiga  kura za kumwondoa Meya Kimbe madarakani limekwenda  vizuri baada ya wajumbe wote 26  kushiriki kupiga kura za  kutokuwa na imani na meya  na  matokeo kura  zilizoharibika ni 12 na  kura  za  hapana hakuna na za  ndio ni 14.

“Hivyo natangaza  rasmi  matokeo ya  kura  zilizopigwa  waliosema ndio  meya  aondoke madarakani wameshinda hivyo natangaza  rasmi  kuwa Alex  Kimbe  kuanzia  leo (jana) Machi 28 mwaka 2020  sio msitahiki meya  tena wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa hadi kufikia hapa kikao  kimefungwa,” alisema Ryata.

Akizungumza baada ya kutangawa kuondolewa madarakani Kimbe alisema yeye bado ni meya wa kwani  kikao hicho kimeshindwa kuffikisha mbili ya tatu  ya wajumbe wote  wote 26 waliopaswa kupiga kura.

“Wameshindwa kunitoa katika nafasi yangu kwa sababu  wameshindwa  kufikisha mbili ya tatu ya wajumbe wote kama  ambavyo kanuni inasema, theluthi mbili wajumbe wote katika Halmashauri ni 17  leo tulikuwa madiwani  26   lakini  ili meya  ama mwenyekiti wa Halmashaurti aweze kuondoka kanuni  ipo wazi  kuwa wajumbe mbili ya  tatu ndio  wanapaswa  kumwondoa  na waliopiga  kura  za  kuniondoa ni  14   ilipaswa  wawe  17 hivyo mimi bado meya “

Aidha  alisema katika  kikao hicho  wakati  ikisomwa taarifa ya matokeo ya  uchunguzi wa  tuhuma dhidi  yake   alinyimwa haki ya kujieleza.

Kwa  upande  wake  Mbunge wa  Iringa  Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, alisema mbinu  ambayo  waliitumia  kupiga kura ni mbinu kabambe ya  kubaini  wasaliti  ndani ya Chadema  baada ya kupata  taarifa za ndani kutoka CCM kuwa  kuna mbinu ya  kuwanunua madiwani watatu ama zaidi ili wapige kura  za kumwondoa meya.

” Tulitaka kura zetu 12  kuwa salama bila kununuliwa lakini wakati huo  huo sio kwamba hizo kura kura 12  hazijapigwa  zimepigwa  hivyo kura zilizopigwa ndani ya ukumbi ni kura 26  na zilizomtaka  meya aondoke ni kura 14 za CCM na 12  ni kura   zilizoharibika.

“Kanuni ipo wazi inamtaka meya  kuondoka kwa theluthi  mbili ya  kura zilizopigwa si vinginevyo, walihitaji kura  nyingine tatu ambazo hawajazipata ” alisema Msigwa .

Kwa upande wa  diwani wa CCM, Nguvu Chengula  na  Ibrahim Ngwada, alisema Chadema walikuwa  wametengeneza mbinu ya kutopiga  kura imekwama baada ya zoezi hilo kufanyika kwa mafanikio.

Alisema kitendo cha madiwani kutopiga kabisa  kura  kimetoa nafasi ya meya  kuondolewa kwani walipaswa  kupiga  kura za  hapana na sio  kutopiga.

Mwanasheria  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa,  Nicholaus Mwwakasungura,  alisema  kitendo ambacho  wamekifanyha  Chadema kutopiga  kura ya hapana ama ya ndio, kimetengeneza mazingira ya  kuonesha kura za hapana  zimeshinda katika mchakato huo.

“Kwa matokeo haya ni wazi  kuanzia Machi 28 Meya  Kimbe ameondolewa madarakani na sio meya tena wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa na anapaswa  kukabidhi  ofisi.
“Imebainika Kimbe anamiliki mali ambazo haziendani na  kipato chake kwani kipato chake  kwa mwaka ni Sh milioni 15  fedha  inayohusisha  posho  za  vikao, posho  ya madaraka, takrimu na posho za vikao na shughuli za kilimo, duka la vipuri na  biashara  ya  wakala wa voda ni vyanzo hafifu vya mapato  ya meya  huyo kuweza  kumiliki mali hizo,” alisema.

Alisema  timu ya uchunguzi ilibaini kuwa anamiliki shamba lenye  ekari 30  lililopo  katika mataa wa Chautinde Kata ya  Isakalilo, shamba la  ekari 35  lililopo Pawaga  ambalo analitumia  katika kilimo cha Mpunga na Shamba  la  ekari tisa lililopo Pawaga ambalo analima mpunga.

Pia alisema anamiliki shamba ekari sita mtaa wa Kitasengwa kata  ya Isakalilo  na mashamba  mengine  yaliyopo  Kilolo  na nje ya  mkoa wa Iringa, nyumba  tatu, gari aina ya Nadia  ambavyo  vyote  hivyo  alipata kati  ya mwaka 2015 na 2020 kipindi  akiwa Meya

Alisema walibaini pia kuwa ana eneo jingine la Chautinde  lenye ekari 25 maeneo hayo yapo  ndani ya kata anayoiongoza ya Isakalilo  Manispaa  ya Iringa.

” Imebainika kuwa meya  Kimbe anamiliki mali  ambazo haziendani na  kipato chake  kwani kipato chake  kwa mwaka ni wastani wa  shilingi milioni 15  fedha  inayohusisha  na posho  za  vikao, posho  ya madaraka,takrimu pamoja  na posho za vikao  na  shughuli za kilimo ,fuka la vipuri na  biashara  ya  wakala wa VODA ni vyanzo hafifu vya mapato  ya meya  huyo kuweza  kumiliki mali hizo .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles