Madiwani CCM, Chadema ‘wazichapa kavukavu’

0
1100

Tunu Nassor, Dar es SalaamMadiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ‘wamezichapa kavukavu’ katika uchaguzi wa Naibu Meya Ilala baada ya Chadema kudai kura zao zimechakachuliwa.

Uchaguzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Anatoglou jijini Dar es Salaam leo Jumatano Oktoba 3, ambapo katika uchaguzi huo, Diwani wa Kata ya Vingunguti, Omar Kumbilamoto (CCM), amefanikiwa kutetea kiti hicho baada ya kushinda kwa kura 27, huku mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Adam Rajabu, akipata kura 25 na Patrick Assenga (Chadema) akiambulia kura 0.

Vurugu hizo zilianza baada ya madiwani kupiga kura na kwenda kuhesabiwa katika chumba cha kuhesabia kura, mgombea wa Chadema alitoka akipiga kelele kuwa CCM wameanza kuharibu uchaguzi.

Baada ya kusema hivyo maaskari waliokuwapo ukumbini hapo waliingia katika chumba hicho, Assenga alidai askari walimwamuru mgombea wa CUF kurudisha kura alizokuwa amehesabiwa mkononi ambazo zilikuwa 27 katika sanduku la kura na matokeo yake kura hizo akapewa Kumbilamoto.

Wakala wa Kumbilamoto baada ya kuhesabiwa kura hizo alitoka akishangilia ambapo alikutana na Assenga akiwa na madiwani wa Chadema akilalamika kuibiwa kura ambapo madiwani hao waliinuka na kuanza kurushiana ngumi na kutoleana matusi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here