24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Madereva mwendo kasi waendesha mgomo baridi

DART-7Ruth Mnkeni na Asifiwe George, Dar es Salaam

MADEREVA  wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka(UDART), jana waliendesha mgomo baridi kwa madai kwamba mshahara wanaolipwa ni mdogo  na haukidhi mahitaji yao.

Mgomo huo ulidumu kwa saa mbili na  MTANZANIA ilishuhudia abiria wengi wakiwa katika vituo mbalimbali kikiwamo cha Kimara Mwisho wakisubiri huduma hiyo.

Magari hayo yanatakiwa kuanza  kutoa huduma saa 11.00 alfajiri ambako madereva wanakuwa wawili kwa kila gari na kila mmoja anatakiwa kufanya kazi kwa saa nane.

Akitoa ufafanuzi kuhusu mgomo huo, Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa,  alisema madereva 30 ambao hawajasaini mkataba ndiyo waliofanya mgomo  na wengine 300  tayari wameshasaini mikataba yao na wanaendelea na shughuli kama kawaida.

Alisema madereva wanatakiwa kulipwa   Sh 800,000 lakini mshahara huo umegawanyika mara mbili ambako kuna Sh 400,000  ambazo hulipwa kila mwezi na kiasi kingine cha Sh 400,000 hulipwa kwa kuangalia kutimizwa kwa vigezo vya masharti ya mkataba.

“Shilingi 400,000 ni kiwango kisichobadilika kwa mwezi lakini  baada ya kupimwa  vigezo sita ambavyo ni usafi, kuwahi kazini, kutopata ajali na kuwahi kwa wakati kutoka kituo kimoja hadi kingine ndiyo hulipwa Sh 400,000 nyingine,”lisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles