24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Madam Rita ajivunia miaka 10 ya BSS, msimu mpya kuanza Septemba 28

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Benchmark Productions na Jaji Mkuu wa shindano la kusaka vipaji Bongo Star Search (BSS), Rita Poulsen ana furaha na anajivunia kufanikiwa kuvumbua vipaji vya kuimba vya vijana mbalimbali nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Septemba 17, wakati wakitangaza msimu mpya wa shindano hilo litakaloanzia mkoani Arusha, amesema BSS imefanikiwa kuwapa nafasi vijana hao wa kitanzania kuendeleza maisha ya kimuziki na wengine kufanikiwa nje ya muziki pia.

“Kwa sababu ni ‘anniversary’ ya miaka 10 ya Bongo Star Search, najivunia vipaji ambavyo tumevileta mbele ya Watanzania na kufanikiwa kueneleza vipaji vyao nje ya muziki.

“Kuhusu ujio wa msimu wa 10 huku akitaja ongezeko la mikoa ambayo itafikiwa na usaili wa shindano hilo, habari njema sana kwa Watanzania ni kwamba tumeongeza idadi ya mikoa ambayo itafikiwa na usaili wa BSS mwaka huu ni Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma na Dar es Salaam,” amesema.

Kwa upande wake Meneja Masoko StarTimes Tanzania, David Malisa, amesema Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes itaonyesha mchakato mzima wa BSS kupitia chaneli ya StarTimes Swahili.

“Huu unakuwa ni msimu wa pili mfululizo kwa shindano hilo kuruka kupitia chaneli hiyo, sisi tunawaamini sana Watanzania kama wao walivyotuamini na kuchagua kutumia huduma na bidhaa zetu, na kwa kuzingatia hilo tunaendelea kubeba uhalisia wa jamii ya kitanzania na aina ya burudani ambayo wamekuwa wakiifurahia kwa miaka 10 sasa, nazungumzia BSS na vimbwanga vyake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles