31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Madaktari waonya kuhusu Assange

LONDON, UINGEREZA

KUNDI la madaktari na wataalamu wa saikolojia wapatao 120 wametoa wito wa dharura, kutaka mwanzilishi wa mtandao wa Wikileaks, Julian Assange, apewe huduma nzuri za afya.

Katika waraka waliouchapisha katika jarida maarifa la kitabibu la The Lancet, wataalamu hao wamesema Assange ambaye hivi sasa yuko jela, amepitia mateso ya kisaikolojia na mahitaji yake kiafya kupuuzwa.

Waliema katika waraka huo kuwa Assange anateseka kutokana na athari za kuzuiliwa kwa muda mrefu katika ubalozi wa Equador mjini London, na baadaye kufungwa katika jela lenye ulinzi mkali la Belmarsh jijini humo.

Kwa mujibu wa wataalamu hao, upo uwezekano wa Assange mwenye umri wa miaka 48 kufia gerezani.

Julian Assange anayetafutwa na Marekani, amekuwa katika gereza la Belmarsh mashariki mwa London tangu Aprili mwaka 2019.

Madaktari hao pamoja na Shirika la Kutetea Haki za Waandishi wa Habari Ulimwenguni (RSF) wanasema mwanzilishi wa mtandao wa Wikileaks, Julian Assange anayeshikiliwa nchini Uingereza anateswa kisaikolojia.

Madaktari hao zaidi ya 100 pamoja na Shirika la Kutetea Haki za Waandishi wa Habari Ulimwenguni, RSF, wanasema Assange anayeshikiliwa nchini Uingereza anateswa kisaikolojia kwa kwa kutopewa huduma bora ya kiafya.

Hayo yamo kwenye barua iliyoandikwa na madaktari na shirika hilo wiki moja kabla ya mahakama ya Uingrereza kuanza kusikiliza kesi ya Assange, ambayo huenda ikaamuwa apelekwe Marekani.

Madakatari hao  pamoja na shirika la waandishi wasiokuwa na mipaka ( Reporters Sans Frontieres) wamelaani mateso ya kisaikolojia anayofanyiwa kiongozi huyo wa mtandao wa WikiLeaks ambaye yuko hatarini kupelekwa Marekani ili kujibu mashtaka ya ujasusi.

Kwenye barua ya pamoja iliyotangazwa kwenye gazeti la kitabibu la Uingereza, The Lancet, kundi hilo la madakatari 117 kutoka nchi 18 wameituhumu serikali ya Uingereza kukanyaga haki za kimsingi za Julian Assange za kupata matibabu.

Tuhuma hizo zimekuja wiki moja kabla  ya mahakama ya Uingereza kusikiliza kesi ya kupelekwa marekani kwa raia huyo wa Australia mwenye umri wa miaka 48, na ambaye ameshikiliwa kwenye gereza ya ulinzi mkali ya Belmarsh, Kusini mwa Jiji la London.

“Ikiwa Assange atafariki ndani ya gereza la Uingereza” kama alivyotahadharisha mjumbe wa umoja wa mataifa kuhusu mateso, Nils Melner mwezi Novemba uliopita, ni wazi kwamba “aliteswa hadi kufa,” welezea madaktari hao.

Toka mwaka wa 2015 ambao Assange alifanyiwa uchunguzi na daktari kwenye ubalozi wa Equador alikokimbilia kwa miaka mitatu kabla, mapendekezo ya madaktari wake ya kupewa huduma bora ya kiafya “yaliendelea kupuuzwa”.

Madktari hao pamoja na shirika la “Reporters Sans FrontieresL wametuhumu kile wanachoelezea kuwa ni “kufanyiwa siasa kwa maadili za kimsingi za kigangas”. Madaktari hao wametoa mwito wa kuachiwa kwa Julian Assange ili apewe huduma bora za kiafya.

Likipinga hatua ya kupelekwa Marekani kwa Julian Assange, kwa kile inachoelezea kwamba Assange ”alitoa taarifa kwa faida ya umma”, shirika la wandishi habari wasiokuwa na mipaka lilikusanya saini 20.000 juzi Jumatatu.

Mwanzoni mwa Novemba, mjumbe maalumu wa wa Umoja wa Mataifa kuhusu mateso, aliliambia shirika la AFP kwamba wasiwasi wake ni kutokana na taarifa za kuaminika kwamba hali ya kiafya ya Assange siyo nzuri.

Assange ambaye alikamatwa na polisi wa Uingereza kwenye ubalozi wa Equadorwa akitafutwa na Marekani kwa makosa ya kuvujisha maelfu ya nyaraka za siri kuhusu jeshi la Marekani na mabalozi wake. Akikutwa na hatia, anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka 175 jela kwa makosa ya ujasusi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles