27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

MADAKTARI BINGWA MUHIMBILI KUHAMISHIWA HOSPITALI YA TEMEKE

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka baadhi ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), kuhamia Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke ili kumudu hali ya ongezeko la wanaotaka huduma bora za afya hospitalini hapo.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kuhamisha Idara ya Magonjwa ya Ndani  Muhimbili kwenda Hospitali ya Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila (MAMC).

Akizungumza katika ziara yake hospitalini hap oleo Jumatatu Januari 15, Mwalimu amesema jambo aliloligundua ni uwepo wa mlundikano wa wagonjwa wanaohitaji huduma.

“Wale madaktari tunaowatoa Muhimbili hasa madaktari bingwa baadhi tutawahamishia hapa ili kusaidiana na madaktari wa Temeke katika kutoa huduma bora kwa watu wengi zaidi.

“Lakini pia serikali iko mbioni kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kujenga jengo la ghorofa nne ambalo litachangia katika kuondoa tatizo la mlundikano wa wagonjwa hospitalini hapo mapema mwaka huu,” amesema.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke Dk Amani Malima mlundikano wa wagonjwa hospitalini hapo unatokana na upungufu wa watumishi katika kuwahudumia wananchi hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles