27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mabusha tatizo la wengi jijini Dar

dk-grace-magembe

NA HADIA KHAMIS-DAR ES SALAAM

UTAFITI uliofanywa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii unaonyesha kuwa wakazi wa Mkoa wa Dar es salam 6800 tayari wamepata athari ya matende na mabusha.

Akizungumza katika zoezi hilo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dk Grace Magembe alisema mpaka sasa tayari watu 104 kwa Mkoa wa Dar es Salaam wameshafanyiwa upasuaji wa mabusha.

Alisema kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa wa mabusha Jijini Dar es Salaam wanatarajia kuwafanyia upasuaji wagonjwa 1000.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa dawa za kinga tiba ya Matende,Minyoo na Mabusha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, alisema kuwa kiwango hicho ni kikubwa sana kwa wakazi wa dar es salaam kwani mpaka sasa watanzania milioni 2.7 wameathirika na magonjwa yasiyopewa kipaumbele ikiwemo ngiri maji pamoja na matende hususani vijijini.

Alisema zoezi la utoaji wa dawa za kinga tiba litatolewa bure ambapo zaidi ya watanzania milioni 4.5 wanatarajiwa kupata kinga tiba hizo.

“Kinga tiba imeanza  kutolewa  Oktoba 25 hadi 29 kwa watu wenye umri kuanzia miaka 5 na kuendelea  kwa kumeza dawa za Mectizan na Albendazole za kukinga na kutibu magonjwa ya minyoo tumbo,mabusha na matende,”alisema Makonda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles