30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mabula atapita bila kupingwa – Dk. Bashiru

Munir Shemweta – WANMM, Mwanza

KATIBU Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally, amesema hatashangaa kuona Mbunge wa Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula, akipita bila kupingwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani kutokana na kazi kubwa aliyoifanya jimboni humo.

Dk. Bashiru alisema hayo juzi, Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, wakati wa mkutano mkuu wa Jimbo la Ilemela kuelezea utekelezaji wa ilani ya chama hicho.

Alisema hakuna haja ya kumnadi tena Dk. Mabula kwa kuwa ana sifa zinazomwezesha kutetea kiti chake.

Dk. Bashiru alisema yeyote anayetaka kuwania nafasi katika jimbo hilo ajue kiti hicho kishakaliwa pamoja na kata zake 19.

“Ole wake anayetaka kupita mlango wa nyuma, chama kina utulivu, sitashangaa Dk. Mabula akipita bila kupingwa,” alisema Dk. Bashiru.

Alionya wabunge wa chama hicho, waliozembea kufanya ziara za kutatua kero za wananchi na kufanya vikao katika majimbo yao kuwa hawatakuwa na ulinzi wakati wa kinyang’anyiro cha kupendekeza majina ya kuwania nafasi hizo.

Aliwaambia wana Ilemela kwa sasa kuna tofauti kubwa ya maendeleo katika jimbo hilo, ikilinganishwa wakati lilipokuwa chini ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kwa upande wake, Dk. Mabula alisema jimbo limepiga hatua kubwa ya maendeleo katika sekta za elimu, afya, maji, mindombinu, uzalishaji, mifugo, viwanda, biashara, utamaduni na michezo, ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Alisema jimbo limefanikiwa kujenga zahanati mbili mpya; Buganda na Lukobe, hospitali ya wilaya na vituo vya afya vya Lumala na Nyamazogo.

Mabula alisema katika sekta ya elimu, walifanikiwa kujenga shule mpya za sekondari za Kayenze, Angeline Mabula na Kisundi huku shule za msingi zikijengwa mbili; Kayenze na Ihalalo.

Katika hatua nyingine, Dk. Bashiru alionya wafanyabiashara wanaotumia lumbesa na vipimo visivyokubalika katika kupima mazao ya kilimo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles