23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MABEKI KATILI WAKUCHUNGWA KOMBE LA DUNIA URUSI

NA BADI MCHOMOLO

ZIMEBAKI siku 12 kuelekea kwenye kivumbi cha michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi ambayo inatarajia kuanza kutimua vumbi Juni 14.

Jumla ya miji 11 itatumika kwa ajili ya michuano hiyo ambayo itafanyika kwa kipindi cha mwezi mmoja hadi Julai 15.

Timu 32 kutoka mataifa mbalimbali zinaendelea kufanya maandalizi ya vikosi vyao ili kuona uwezekano wa kuandika historia kwa kutwaa taji hilo.

Ubora wa wachezaji pamoja na mifumo ya makocha ndiyo chachu ya mafanikio ya timu kutwaa taji hilo, hivyo kila kocha ametaja kikosi chake chenye wachezaji ambao wamekamilika kuanzia safu ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji.

Timu ambayo itakuwa na ubora katika safu ya ushambuliaji na ulinzi inaweza kufanya vizuri na kuandika historia, wafuatao ni baadhi ya mabeki wanaotajwa kuwa katili na wakuchungwa kwenye michuano hiyo.

Sergio Ramos (Hispania)

Ana umri wa miaka 32, ni miongoni mwa wachezaji wenye uwezo mkubwa na msaada kwa timu yao hasa katika safu ya ulinzi, amekuwa na uzoefu wa michuano hiyo mikubwa.

Atakuwa anakiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Hispania katika safu ya ulinzi, anatajwa kuwa miongoni mwa mabeki katili kwa kipindi hiki.

Mei 26, mchezaji huyo wa klabu ya Real Madrid, alilifanya jina lake lisikauke kwenye midomo ya watu baada ya kumchezea vibaya mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah.

Zaidi ya mashabiki 500,000 walisaini pendekezo la kuwaomba Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) na Chama cha Soka Ulaya (UEFA), achukuliwe hatua kutokana na kitendo chake, hivyo ni mmoja kati ya mabeki wa kuchungwa huko Urusi kwenye Kombe la Dunia.

Thiago Silva (Brazil)

Ni beki wa kati wa klabu ya PSG pamoja na timu ya taifa ya Brazil, amekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya klabu hiyo pamoja na timu ya taifa.

Anatajwa kuwa miongoni mwa mabeki wenye akili nyingi wakiwa uwanjani kwa kucheza mpira kwa umakini wa hali ya juu.

Mbali na upole wa mchezaji huyo, lakini anatajwa kuwa miongoni mwa mabeki katili.

Pepe (Ureno)

Miongoni mwa mabeki ambao walikuwa na mchango mkubwa katika klabu ya Real Madrid misimu iliyopita ni pamoja na Kepler de Lima maarufu kwa jina la Pepe.

Kwa sasa mchezaji huyo anakipiga katika klabu ya Besiktas baada ya kuondoka Madrid, mchezaji huyo yupo kwenye kikosi cha Ureno kuelekea Kombe la Dunia nchini Urusi. Pepe ni mmoja kati ya mabeki wenye roho mbaya na amekuwa akioneshwa kadi za njano na nyekundu mara kwa mara kutokana na ukatili wake.

Vladimir Granat (Urusi)

Wenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia timu ya taifa ya Urusi wanaamini safu yao ya ulinzi ipo sehemu salama kutokana na ubora wa beki wao wa kati, Granat.

Beki huyo anakipiga katika klabu ya Rubin Kazan, inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo, amekuwa akihakikisha ulinzi kwa timu yake kwa kuwafanya washambuliaji wasipate nafasi ya kupita.

Nicolas Otamendi (Argentina)

Amekuwa na mchango mkubwa katika klabu ya Manchester City msimu huu, ameweza kuwadhibiti wapinzani na kuifanya timu hiyo ichukue ubingwa wa Ligi Kuu England.

Kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kimempa mchezaji huyo jukumu la kulibeba taifa kwenye michuano ya Kombe la Dunia kwa kuweka ulinzi imara kama alivyofanya ndani ya Man City.

Diego Godin (Uruguay)

Katika kikosi cha Atletico Madrid, mchezaji huyo amekuwa akisimama vizuri kwenye nafasi yake ya ulinzi hadi timu hiyo inamaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi nchini Hispania.

Kutokana na ubora wake na umakini katika safu ya ushambuliaji, mchezaji huyo atakiongoza kikosi cha Uruguay kwa kuweka ulinzi kwa mlinda mlango wake.

Samuel Umtiti (Ufaransa)

Mchezaji huyo alimfanya beki wa kati wa Barcelona, Gerard Pique, kuwa na wakati wa kupumzika kutokana na ubora wake.

Mara nyingi alionekana kupambana na washambuliaji kwenye michuano ya Ligi Kuu nchini Hispania na kufanikiwa kutwaa ubingwa, alikuwa anaonekana kuwa na roho mbaya uwanjani hasa kutokana na rangi yake nyeusi, hivyo Ufaransa wanaamini wapo sehemu salama kwa uwepo wa mchezaji huyo.

Cristian Zapata (Colombia)

Klabu ya AC Milan iliwahi kuwa na beki mwenye roho mbaya miaka ya nyuma akijulikana kwa jina la Gennaro Gattuso, lakini kwa sasa yeye ni kocha wa timu hiyo.

Beki ambayo anatajwa kuchukua baadhi za tabia za mchezaji huyo ni Cristian Zapata raia wa nchini Colombia, hivyo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, amepewa jukumu la kuwazuia washambuliaji ambao watakuwa na nia ya kuwafunga kwenye michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi.

Raphael Varane (Ufaransa)

Mwonekano wake akiwa uwanjani ni kama mpole sana huku miguu yake ikiwa na matege, lakini amekuwa akiimarisha ulinzi katika kikosi cha Real Madrid pamoja na timu ya taifa ya Ufaransa, amekuwa akipambana na washambuliaji wenye kasi kwa kuwachezea vibaya, hivyo atakuwepo kwenye Kombe la Dunia nchini Urusi. Hao ni baadhi ya mabeki wa kuangaliwa kwenye Kombe la Dunia mwaka huu

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles