28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MAAMBUKIZI YA MALARIA  YAPUNGUA MWANZA

Na JUDITH NYANGE

MKOA wa Mwanza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya umefanikiwa kupunguza kwa asilimia nne vifo vinavyotokana na   malaria kutoka asilimia 19.1 katika   miaka mine.

Vifo hivyo vimefikia asilimia 15 mwaka 2015/16 kutoka asilimia 19 za mwaka 2011/12.

Mganga Mkuu wa Mkoa waMwanza, Dk. Leornard Subi, alikuwa akizungumza wakati wa kugawa  vyandarua kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Senge,   Kata ya Bujashi  wilayani Magu ikishuhudiwa na wajumbe  wa Bunge la   Marekani.

Dk. Subi alisema mwaka 2011/12 kiwango cha maambukizi ya malaria mkoani Mwanza kilikuwa   asilimia 19.1 lakini  kwa mujibu wa utafiti uliofanyika hadi kufikia mwaka 2015/16 kiwango hicho kimepungua na kufikia asilimia 15.

Alisema   wanaoathirika zaidi ni wanawake wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano.

Katika mapambano dhidi ya malaria makundi hayo yamepewa kipaumbele cha  pekee, alisema.

Alisema  mkoa umeanzisha progaramu ya  ugawaji wa vyandarua katika vituo vya afya, hospitali, zahanati na kwenye shule kwa wanafunzi wa darasa la kwanza, nne, tano na sita  unaotekelezwa na serikali  kwa kushirikiana na Shirika la  Msaada la Marekani (USAID).

“Hatudhibiti malaria kwa chandarua pekee yake tunatumia njia mbalimbali  ikiwamo kuwapatia tiba sahihi na kamili kwa wagonjwa wanaogundulika kuwa na malaria, kugawa dozi zaidi ya tatu za SP kwa wajawazito ili kudhibiti vimelea vya malaria.

“Kwa sababu akipata ugonjwa huu anakuwa katika hatari ya kupoteza damu nyingi ambayo inaweza kumsababishia kifo.

“Malaria ni hatari kwa sababu mtu akipata  vimelea vyake vinashambulia chembechembe nyekundu za damu ambapo inaweza ikaathiri figo, mwili kudhoofika, na baadaye husababisha mgonjwa kuishiwa damu,” alisema Dk. Subi.

Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka USAID, Chriss Thomas, alisema  alifurahishwa na juhudi na mafanikio makubwa yaliyofikiwa na  serikali ya Tanzania katika kupambana na malaria.

Aliahidi kusaidia zaidi mapambano hayo kuokoa maisha ya wajawazito na watoto walio kwenye hatari zaidi kutokana na ugonjwa huo.

Wilaya za  Ukerewe na Buchosa ndizo zinazoongoza kwa kuwa na maambukizi makubwa ya malaria ambako   vyandarua zaidi ya 500,000 vimegawanywa katika shule 941, zahanati, vituo vya afya na hospitali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles