24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Maajabu ya ajali ya basi na lori Dar

Basi la Safari Njema lililoteketea kwa moto baada ya kugongana na lori eneo la Kimara Stop Over Dar es Salaam jana. PICHA NDOGO: Magari hayo yakiteketea.
Basi la Safari Njema lililoteketea kwa moto baada ya
kugongana na lori eneo la Kimara Stop Over Dar es Salaam jana. PICHA NDOGO: Magari
hayo yakiteketea.

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

BASI la Safari Njema  namba   T 990 AQF linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Dodoma, limeteketea kwa moto baada ya kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa limebeba saruji ambalo nalo liliteketea kwa moto.

Ajali hiyo iliyotokea jana jioni eneo la Kimara Stop – Over,  Dares Salaam,  imeacha simanzi huku wananchi waliokuwa kwenye eneo la tukio wakiangua vilio kwa hofu ya abiria waliokuwa ndani basi hilo kuteketea kwa moto.

Habari zinasema  lori hilo namba   T 534 BYJ  liliteketea kwa moto na kubaki  tela tu.

Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo,  Denis Atiris, alisema ajali hiyo ilitokea saa 8:20 mchana baada ya lori kukosa mwelekeo na   kuligonga basi hilo la abiria.

“Lile lori lilionekana kukosa mwelekeo, lilikuwa linatoka mjini kuelekea Mbezi,  lilionekana likiyumba kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

“Dereva wa basi alikuwa anatoka kituo cha Gereji   ambako aliingia kushusha abiria.  Wakati anatoka kituoni kuingia barabarani ndipo akaona lori likiyumba,  ikabidi alikwepe kwa kutoka kidogo nje ya barabara ili wasigongane uso kwa uso.

“….kwa bahati mbaya lile lori lilikwenda moja kwa moja kugonga sehemu ya ubavuni mwa basi, kukawa na kishindo kikubwa na ghafla moto ukaanza kuwaka ndani ya basi,” alisema Atiris.

Shuhuda huyo alisema kitendo hicho kilitokea   ndani ya sekunde chache na  baadhi ya abiria waliokuwa ndani ya basi walionekana wakiruka nje kupitia madirishani.

“Ikabidi mimi na mwenzangu anayeuza maua hapa jirani na kituo, tuingie ndani wakati huo moto ulikuwa… si mkubwa sana, tukafanikiwa kuwatoa watoto watano na wa-dada wanne,” alisema.

Alisema hata hivyo hawakuweza kuokoa wengi zaidi kwa vile moto ulizidi kuongezeka baada ya kama dakika 15.

Saruji yaibwa

“Watu waliongezeka kadri muda ulivyosonga lakini jambo la kusikitisha ni kwamba hawakuja kusaidia kuokoa badala yake walikimbilia simenti (saruji) iliyokuwa kwenye lori wakaanza kuiba,” alisema na kuongeza:

“Kwa kweli kitendo kile kimenisikitisha mno, watu tumekosa uzalendo na utu kabisa, tungesaidia  tungeweza kuokoa wengi”.

Atiris alisema hata hivyo hakumbuki idadi ya abiria waliokuwamo ndani ya basi hilo.

“Gari la kwanza lililofika eneo la tukio ni la polisi ambao walitusaidia kubeba wale majeruhi na kuwawahisha hospitalini, walitupa ushirikiano mzuri.

“Lakini jambo linalonisikitisha ni hawa wa Zimamoto, tangu saa 8:20 wamekuja saa 11:20 gari lote likiwa limeshateketea kwa moto na hakuna kitu kilichosalimika,” alisema shuhuda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles