24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Maadili yanaporoka sekta ya afya

KWA muda sasa, kumekuwapo na matukio ya ajabu yanayotokea sekta ya afya ambayo hakika yanasikitisha na  kutia huruma.

Tumepata kuandika na kutoa ushauri juu ya wahudumu wa afya namna wanavyokumbwa na matukio ya kusikitisha wanayofanyia wagonjwa sehemu zao za kazi.

Matukio haya mara nyingi yanafanywa na wauuguzi walio zamu nyakati za usiku. Matukio yenyewe ya kubaka wagonjwa kwa nguvu, jambo ambalo linakwenda kinyume na maadili ya kazi.

Tunakumbuka  miezi michache iliyopita, tumeandika na kulaani vikali tukio la muuguzi katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga aliyebaka mgonjwa kwa nguvu ofisini, kisha akakimbia mpaka sasa hatujasikia kama ametiwa mbaroni.

Matukio ya aina hii yanasikitisha mno na kusononesha jamii ukizingatiwa watu wanakwenda hospitali kupata huduma ya tiba, lakini wanapofika wanakutana na unyama ambao hakuutegemea.

Kwa mfano katika tukio la Igunga, mkoani Tabora, muuguzi alifanya unyama huu wakati akimhudumia mgonjwa mwenye umri wa miaka 16 ambaye hakika ni mtoto mdogo, lakini tunasikitika mpaka sasa hakuna chombo cha dola kilichomtia mbaroni.

Hatuelewi kwanini imechukua muda mrefu kiasi hiki, polisi kumatia mbaroni.

Leo tumelazimika tena kuandika na kulaani vikali tukio la mkazi wa wa Kijiji cha Majimoto wilayani Mlele mkoani Katavi, jina lake tumelifadhiwa mwenye umri wa miaka 22 kudaiwa kubakwa na na muuguzi wa   wa kituo cha afya Mamba, Abednego Alfred (32).

Muuguzi huyu ambaye sasa anashikiliwa na jeshi la polisi baada kutenda kosa hili, anadaiwa kumbaka mjamzito ndani ya chumba cha  kujifungulia.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi,Benjamin Kuzaga  anasema tukio hilo la kinyama na la kikatili  lilitokea Desemba  18, mwaka huu saa 2 usiku

 Anasema siku ya tukio, mwanamke huyo  alipatwa na uchungu wa kujifungua, baada ya siku zake kutimia, alitoka nyumbani kwake Majimoto  kwenda kupata huduma kituoni hapo, akisindikizwa na mama yake mzazi .

Baada ya kufika kituoni alipokelewa na    Alfred ambaye aliyekuwa muuguzi wa zamu siku hiyo na kuanza kumpatia huduma zote zinazotakiwa.

Anasema cha ajabu, badala ya kutimiza wajibu wake akaanza kumwingilia mwathirika wa tukio hili katika mazingira ya ajabu na kumfanya ashituke .

Anasema  baada ya kubaini hilo, licha ya kuwa hatua za mwisho kujifungua alipiga kelele kuomba msaada na kuamua  kutoka kitandani  na kwenda  moja kwa moja  kutoa taarifa  kwa  mama yake mzazi, Mektilida  Deogratius  ambaye alitoa taarifa kwa uongozi wa kituo.

Mtuhumiwa baada ya kufanya kitendo hicho, alitokomea kusikojulikana, lakini polisi kwa kushirikiana na walifanikiwa kumkamata.

Hatukubaliana na unyama huu hata kidogo ndiyo maana tunaitaka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuchukua hatua kali dhidi ya wauguzi wenye tabia za  aina ili liwe funzo kwa wengine.

Tunalipongeza jeshi la polisi na wananchi kwa kazi kubwa ya kumsaka na kumkamata mtuhumiwa huyu ili afikishwe mahakani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Siku zote tunaamini, wauguzi au watumishi wa umma wana taratibu,sheria na kanuni zinazowaongoza, sasa inakuwaje wanatoka kwenye mstari kiasi hiki? Kuna tatizo ama kutoka kwa wakubwa waoa wanao wasimamia hawatimizi wajibu wa kufanya vikao vya mara kwa mara kuzungumza nao.

Kwa msingi huo, tunatoa raia  waganga wakuu wa mikoa, wilaya na zahanati kufanya vikao na watumishi wao wa chini ili kuondoa aibu hii ambayo sasa inaonekana wazi kuona mizizi kadrii siku zinavyokwenda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles