24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MA-RPC KUJADILI MBINU MPYA KUPAMBANA NA UHALIFU

Na Mwandishi Wetu – Dodoma

MAOFISA wakuu wa Jeshi la Polisi nchini wanatarajia kukutana mkoani hapa kuanzia kesho kwa kikao kazi cha siku tatu kujadili na kupanga mikakati ya kukabiliana na uhalifu na wahalifu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Advera Bulimba, alisema kikao hicho kitawakutanisha maofisa wakuu wa makao makuu ya polisi, makamanda wa polisi wa mikoa na wa vikosi Tanzania bara na Zanzibar.

Alisema kikao hicho kitajadili mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika utendaji kipindi cha mwaka uliopita na kuweka mikakati mipya ya kupambana na uhalifu kwa mwaka 2017.

Aidha, Bulimba alisema mbali na utaratibu wa mawasiliano ya kila siku, Jeshi la Polisi pia lina utaratibu wa kukutana kila mwaka ili kubadilishana uzoefu katika kukabiliana na wahalifu, kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika.

“Katika kikao hicho, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu, atatoa maelekezo ya kiutendaji ambayo lengo lake ni kuhakikisha kila ofisa, mkaguzi na askari anawajibika kwa nafasi yake katika kuhakikisha uhalifu unapungua hapa nchini,” alisema.

Bulimba alisema kikao kazi hicho kinatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ambapo kaulimbiu ni ‘zingatia maadili tunapopambana na uhalifu ili kuimarisha usalama kwa maendeleo ya taifa”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles