31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

LWANDAMINA APEWA RUNGU KUIMALIZA ZANACO

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM


BENCHI la ufundi la timu ya Yanga, limempa majukumu kocha mkuu George Lwandamina, kuhakikisha taarifa za ndani za wapinzani wao Zanaco ya Zambia zinapatikana kabla ya kukutana nao katika mchezo wa raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Yanga imefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuwaondosha wapinzani wao Ngaya de Mde Club katika hatua ya awali ya michuano hiyo kwa kuifunga jumla ya mabao 6-2, ikiwa ni ushindi wa 5-1 ugenini na kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani.

Akizungumza baada ya mchezo wa marudiano dhidi ya Ngaya de Mde uliochezwa juzi katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, alisema wanakutana na timu kubwa yenye upinzani hivyo ni lazima wajipange sawasawa ili waweze kuvuka raundi hiyo.

“Tunfahamu kwamba kocha Lwandamina alishawahi kuifundisha Zanaco miaka ya nyuma, lakini hatuwezi kusema mchezo wetu dhidi yao utakuwa rahisi isipokuwa tutamuomba asaidie kupatikana kwa taarifa zao ili iwe kazi rahisi kupambana nao,” alisema.

Mwambusi alisema licha ya timu yao kupata mafanikio na kutinga raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wachezaji walikosa umakini na kupoteza nafasi zao nyingi katika mechi ya marudiano na kusababisha matokeo ya sare ya bao 1-1.

Akizungumzia pambano la watani wa jadi litakalopigwa Jumamosi hii, Mwambusi alisema wameanza kujipanga ili waweze kupata matokeo mazuri yatakayowarejesha kileleni kwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwa sasa Yanga inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kujikusanyia pointi 49, huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi, wakati Simba inaongoza usukani kwa kufikisha pointi 51.  

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles