27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

LWANDAMINA APATA MTIHANI MPYA YANGA

NA ZAINAB IDDY


KIWANGO cha juu kilichoonyeshwa na beki, Mwinyi Haji, katika michuano ya Chalenji, ni wazi kimemweka katika wakati mgumu kocha wa Yanga, George Lwandamina wa kuamua kama amrudishe kikosi cha kwanza au aendelee kumsotesha benchi.

Haji aliisaidia timu ya soka ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ kufika fainali ya michuano ya Chalenji inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), iliyofikia tamati juzi Jumapili kabla ya kutolewa na wenyeji Kenya kwa mikwaju ya penalti 3-2.

Katika michuano hiyo, Haji alionyesha kiwango cha hali ya juu, kiasi cha kuzua mijadala miongoni mwa wadau wa soka hususani mashabiki wa Yanga ambao wanaona anastahili kuwa miongoni mwa wachezaji 11 wa timu hiyo wanaoanza na  Gadiel Michael.

Tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Lwandamina amekuwa alimwanzisha Michael aliyesajiliwa kutoka Azam FC kucheza nafasi ya beki wa kushoto badala ya Haji, aliyekuwa akitumika msimu uliopita.

Lakini sasa kiwango cha hali ya juu kilichoonyeshwa na Haji katika mashindano ya Chalenji ni mtego kwa kocha huyo raia wa Uholanzi.

 

 

Akizungumza na MTANZANIA, Mwinyi alimshukuru kocha wa Zanzibar Heroes, Hemed Morocco, kumpa nafasi katika kikosi chake, kwani imemwezesha kuonyesha hadharani kama kiwango chake kimeshuka au la.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles