Lulu: Changamoto zimenifunza

0
1756

THEREZIA KIBAJA (TUDARCo)

MWIGIZAJI maarufu nchini, Elizabeth Michael, anayejulikana kwa jina la Lulu, amesema amejifunza mambo mengi kutokana na changamoto mbalimbali alizopitia kwenye maisha yake.

Akizungumza na MTANZANIA jana, msanii huyo ambaye amefanikiwa kutwaa tuzo mbalimbali kama vile mwigizaji bora wa kike kutoka Zanzibar International Film Festival, filamu bora ya Afrika Mashariki kutoka Africa Magic Viewers Choice, alisema maisha aliyopitia yamemfanya abadilike kwa kiasi kikubwa.

“Nimebadilika sana, naweza kufanya maamuzi kwa kuangalia jicho la pili na kwa umakini wa hali ya juu kuliko mwanzo, changamoto na mapito mbalimbali kwenye maisha yangu zimenisaidia sana kukua kiakili na kupata faraja ya kuwajua marafiki wa kweli waliokuwa na mimi kipindi hicho.

“Nina amini kila jambo linakuja kwa sababu katika maisha ya mwanadamu yeyote, hivyo ni vizuri kutumia changamoto hizo kujifunza,” alisema Lulu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here