LULU AKANA KUSABABISHA KIFO CHA KANUMBA

0
526

Msanii maarufu wa filamu, Elizabeth Michael maarufu Lulu (22), amedai kuwa hajasababisha kifo cha msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba bali yeye ndiyo alipigwa kwa panga na marehemu.

Lulu ametoa ushahidi wake leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, mbele ya Jaji Sam Rumanyika ambapo amedai Kanumba alikuwa mpenzi wake na uhusiano wao wa kimapenzi ulianza miezi minne kabla ya kifo chake.

Amedai kuwa katika kipindi chote cha uhusiano wao marehemu alikua akimpiga mara kwa mara na siku ya tukio alimpiga sehemu mbalimbali za mwili kwa kutumia panga zikiwamo mapajani.

Katika ushahidi wake huo Lulu amedai kuwa siku hiyo kabla ya tukio Aprili 6, mwaka 2012 ambayo ilikua Ijumaa Kuu, saa mbili usiku alitoka nyumbani kwao na kwenda nyumbani kwa rafiki zake mikocheni na walipanga kwenda disco kwa ajili ya kusheherekea mkesha wa sikukuu ya pasaka.

“Wakati niko na rafiki zangu, Kanumba alikuwa akinisumbua kwa simu niende nyumbani kwake Sinza hadi nikalazimika kuwaaga rafiki zanguili niende kwake,” amedai Lulu.

Lulu alipandishwa kizimbani Aprili 2012 na kusomewa shtaka la kumuua bila kukusudia Kanumba ambaye pia ni msanii mwenzake.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here