23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Lukuvi: Wadaiwa sugu tutawafungia ofisi na kuziuza hadi mlipe madeni

Anna Potinus

Waziri wa ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi amewataka wadaiwa sugu kulipa madeni wanayodaiwa kabla ya Juni 21 ili kuepuka aibu na fedhea lakini pia kuepuka mkono wa sheria

ambapo amesema baada ya muda uliotajwa kuisha wadaiwa watakaoshindwa kulipa madeni yao taratibu za kisheria zitachukuliwa.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Juni 11 wakati akizungumza na wakuu wa taasisi na mashirika 207 yanayodaiwa kodi ya pango la ardhi zaidi ya shilingi bilioni 200 katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Hazina Mkoani Dodoma ambapo amesisitiza kuwa ulipaji wa kodi ya pango la ardhi sio jambo la hiari.

“Wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi pamoja na majukumu yake mengine inalo jukumu la kukusanya maduhuli yatokanayo na kodi ya pango la ardhi na pia kuchukua hatua za sheria kwa mujibu wa sheria ya ardhi sura ya 113 dhidi ya wadaiwa wanaokataa kulipa kodi hii,”

“Hatu hizi ni pamoja na kubadilisha mmiliki, watu wasiolipa bila kujali ni taasisi gani tunampelekea rais na kubadilisha mmiliki pia kuwafikisha wadaiwa sugu mahakamani zoezi litakaloanza Juni 21, kukamata na kuuza mali kupitia madalali ambao tumeshawateua,” amesema.

Aidha amesema kuwa kumekuwa na upotovu juu msamaha wa kodi ya pango la ardhi kwa taasisi na mashirika ya umma yanayotoa huduma kwa jamii, kulingana na tangazo alililitoa Julai 2018 na hivyo kuwataka wanafikiri wanastahili kupata msamaha kutafuta tangazo la serikali namba 347 la Aprili 26 mwaka huu ambao limefafanua vizuri juu ya msamaha huo.

Amesema hadi ifikapo Juni 21 kwa wadaiwa ambao hawatakuwa wamekamilisha kulipa madeni hatojali ni masikini, tajiri, mheshimiwa, kampuni ya serikali, bali watafunga ofisi, kutakamata magari yao hata kwa wale wanaoishi kwenye nyumba za serikali watazikamata ilimradi walipe kodi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles