22.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

LOWASSA AWAKARIBISHA WALIOKATWA CCM

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amewakaribisha makada wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliokatwa katika uchaguzi kujiunga na Chadema.

Wiki iliyopita Kamati Kuu ya CCM na baadaye Halmashauri Kuu, vilipitia majina 1,400 ya walioomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Wilaya za CCM ambazo ni sawa na zile za kiserikali na kufanikiwa kuchuja hadi kufikia 161.

Akitangaza maazimio ya Halmashauri Kuu ya chama hicho, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, alitaja wilaya tano, zikiwamo Siha, Moshi Mjini, Hai na Makete, kuwa hazikupata wagombea wenye sifa kutokana na kasoro nyingi za kimaadili na kikanuni zilizojitokeza.

Kutokana na uamuzi huo, Polepole alisema wilaya hizo zitaanza upya mchakato wa uchaguzi katika ngazi hiyo.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Lowassa alisema: “Nimesoma na kusikia baadhi ya waliokuwa viongozi katika Chama Cha Mapinduzi wamekatwa ama kutetea nafasi zao au kugombea, kwa sababu mbalimbali. Na jina langu limekuwa likiendelea kutajwa tajwa humo.

“Mimi nawaambia hawa Watanzania wenzetu waliokatwa huko CCM nawakaribisha huku Ukawa wafurahie demokrasia.

“Huku niliko kuna maisha mazuri ya kisiasa, uhuru wa fikra na demokrasia halisi,” alisema Lowassa, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.

Mbunge huyo wa zamani wa Monduli alisema Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere alisema ni wakati mwafaka kwa Tanzania kuwa na mfumo wa vyama vingi.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles