27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Lopetegui na mtihani mgumu kuiunda  Real Madrid mpya

ADAM MKWEPU NA MITANDAO

MASHABIKI wa timu ya Real Madrid wameshindwa kuwa na majibu sahihi kwa kile kinachoisumbua timu yao kwa sasa.

Licha ya kuwa katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Hispania, La Liga, lakini bado hawana uhakika wa kufanya kile walichokifanya katika misimu kadhaa iliyopita.

Katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid, imeweka rekodi ya kutwaa taji hilo mara tatu mfululizo baada ya kutwaa msimu uliopita.

Lakini imani yao kwa kocha mpya Julen Lopetegui, imekuwa dhaifu ukilinganisha na ilivyokuwa kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Zinedine Zidane.

Lakini mchezo wa soka unaonekana kuwa hauna kumbukumbu.Iwe kwa sasa au kwa wakati uliopita.

Kwa sasa kila mmoja anazungumzia watu waliondoka katika kikosi cha Real Madrid baada ya michezo mitatu kufanya vibaya.

Wiki mbili zilizopita Real Madrid ilionekana kucheza kitimu zaidi dhidi ya wapinzani wao Altetico Madrid bila kutegemea mchezaji mmoja kama ilivyokuwa kipindi cha Ronaldo.

Lakini michezo mitatu baadaye Espanyol iliwafunga vijana hao wa Lopetegui na hakuna aliyekumbuka kilichotokea dhidi ya Roma katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya au kukumbuka kuwa timu hiyo inalingana pointi 14 na vinara Barcelona katika  msimamo wa Ligi Kuu Hispania.

Mwaka mmoja uliopita Ronaldo akiwa uwanjani huku Zidane akiongoza benchi la ufundi Real Madrid ilikuwa ikihahaha katika michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ikipoteza dhidi ya Tottenham Hotspur katika Uwanja wa  Wembley, England na kupitwa pointi saba dhidi ya Barcelona, LaLiga.

Hali hiyo ilitokea katika michuano ambayo Real Madrid ilishinda kwa mara ya tatu mfululizo.

Lakini changamoto  anayokumbana nayo Lopetegui kwa sasa ni kuiongoza timu ambayo mashabiki na viongozi wake wanataka kufanya vizuri katika kila wakati.

Kitendo cha kushindwa  kufunga katika michezo mitatu iliyopita kimeongeza hofu katika kikosi hicho labda huenda kocha huyo akawa anajadiliwa kufukuzwa.

Kwa sasa kila shabiki ana hoji kuhusu kiwango cha timu hiyo hata hivyo bado wanapaswa kusubiri licha ya kukosa imani naye.

Jambo jingine ni kwamba, Mariano Diaz, hakusajiliwa katika kikosi cha  Real Madrid ili kuziba pengo la Ronaldo kabla ya kocha kumshawishi na kumpa nguvu ya kuamini kwamba anaweza kuvaa viatu hivyo ambavyo havimtoshi.

Majukumu ya Mariano hayafanani na  yale aliyokuwa nayo Ronaldo wakati akicheza  ndani ya kikosi hicho.

Jambo hilo pia linawafanya mashabiki wa timu hiyo kushindwa kumsahau  mreno huyo ambaye aliamua kuondoka bila Real Madrid kupata mbadala wake na kuifanya timu hiyo kuendelea kuugua  ugonjwa wa kukosa mabao msimu huu.

Kipigo cha bao 1-0 walichokipata wiki iliyopita dhidi ya CSKA Moscow katika mchezo wa Ligi ya Mbaingwa Ulaya kiliongeza hasira za mashabiki wao na kuzidi kumkumbuka  Ronaldo.

Wakiwa  na washambuliaji  kama vile Marco Asensio, Karim Benzema na Lucas Vazquez Real Madrid ilishindwa kutamba  dhidi ya wapinzani wao na kujikuta ikiruhusu kupoteza mchezo huo.

Tayati kocha Lopetegui ameshindwa kutwaa kombe la Super Cup wakati walipovaana na  Atletico Madrid na kupoteza kwa mikwaju ya penalti 4-2.

Gazerti la Mundo Deportivo la nchini Hispania limeelezea kuwa   kuporomoka   kiwango cha wachezaji wa timu hiyo kunakuja baada ya kocha huyo  kukosa  ubora wa nyota wake watano wa kikosi cha kwanza  akiwamo  Luka Modric, Gareth Bale, Keylor Navas, Marcelo na Mariano.

Hata hivyo mbali ya kuoneakana kuchoka na umri kuwa mkubwa lakini gazeti hilo linaongeza kuwa wachezaji hao hawaelewi wanachofundishwa na kocha huyo.

Sababu hiyo ndiyo ilimfanya Marcelo kuwa na hasira hata baada ya kupoteza mchezo  dhidi ya Girona ambao ulichezwa Agosti mwaka huu ambao Madrid ilifungwa mabao 4-1.

Hata viongozi wa klabu hiyo pia hawaonekani kuwa na furaha kutokana na mambo yanayoendelea katika benchi la ufundi la timu hiyo wakati Bale akiathiriwa na kitendo cha kutumika kama mchezaji wa akiba wakati wa michezo ya kwanza ya msimu.

Wakati hayo yote yakiendelea kipa Keylor Navas yupo katika lindi la mawazo kuhusu hatima yake hasa baada ya  ujio wa kipa Thibaut Courtois  aliyejiunga na timu hiyo akitokea Chelsea.

Mundo Deprtive pia lilieleza kuwa Mariano bado ana hasira ya kutumika kama mchezaji wa akiba huku akimwangalia Benzema  akiendelea kucheza kama mchezaji wa kikosi cha kwanza tangu September  mosi mwaka hu.

Kutoka na hali hiyo Lopetegui amejikuta katika wajkati mgumu kuunda Real Mdrid mpya itakayokuwa  zaidi ya  kile ambacho kiliongozwa na  Zidane.

Klabu hiyo hadi sasa imeshindwa kuinasa saini ya Paul Pogba,  Neymar Jr na Eden Hazard ambao wealitarajiwa kuwa mbadala wa Ronaldo.

Hata hivyo inadaiwa kuwa klabu hiyo ina mpango wa kuwarudia katika dirisha dfogo la usajili Januari mwakani.

Lakini klabu hiyo huenda ikafanya uamuazi mgumu wa kuajili kocha mwingine kama hali ikiendelea kuwa ngumu kwa aliyekuwa sasa.

Mwaka 2015 klabu hiyo ilimuajili kocha Rafa Benitez  akitokea Napoli lakini  alifukuzwa  baada ya kukaa chini ya mwaka mmoja katika klabu hiyo.

Baada ya kuondoka nafasi yake ilichukuliwa na Zinedine Zidane,  ambaye aliipata klabu hiyo ubingwa  wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mara tatu kabla ya kuondoka Mei mwaka huu.

Akiulizwa kama timu hiyo ipo katika hali mbali wqakati ikijiandaa kuvaana na Alaves, jumamosi iliyopita  Lopetegui anasema: “Hatujadili  mambo ambayo watu wanafikiria, tumachofanya ni kuangilia kitu cha muhimu tunachotakiwa kufanya ili timu ikae sawa.

“Kwa sasa tunajikita zaidi katika mi[pango ya kuhakikisha tunafanya vizuri kama timu nyingine zinazofanya.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles