33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Liverpool kumkosa Alisson wiki mbili

LIVERPOOL, ENGLAND

KOCHA wa timu ya Liverpool, Jurgen Klopp, amethibitisha kuwa,  wataikosa huduma ya mlinda mlango wao Alisson Becker kwa wiki mbili baada ya kuumia katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Ligi Kuu England dhidi ya Norwich City mwishoni mwa wiki iliopita.

Katika mchezo huo, Liverpool walifanikiwa kuanza vizuri kwa ushindi wa mabao 4-1, lakini mlinda mlango huyo alipata tatizo la nyama za paja kipindi cha kwanza cha mchezo huo na nafasi yake ikachukuliwa na kipa namba mbili Adrian Castillo.

Baada ya kufanyiwa vipimo vya awali, kocha Klopp ameweka wazi kuwa, tatizo la mchezaji huyo linaweza kufanya akawa nje ya uwanja kwa wiki mbili.

“Sio majeraha makubwa sana, tatizo la nyama ambalo linaweza kumfanya akawa nje ya uwanja kwa wiki mbili, sitaki kulizungumzia sana suala hilo, lakini ukweli ni kwamba ataikosa baadhi ya michezo ikiwa pamoja na ule wa Jumatano dhidi ya Chelsea wa Uefa Super Cup, lakini hali ya kipa huyo itategemea.

“Mwanzo niliona kama atakaa nje ya uwanja kwa wiki sita, lakini tatizo lake sio kubwa sana kama nilivyodhani, lakini tunatakiwa kusubiri na kuona hatima yake,” alisema kocha huyo.

Hata hivyo, kocha huyo anaamini mlinda mlango namba mbili Adrian, ataongoza michezo hiyo inayofuata ikiwa ni siku tisa tangu ajiunge na kikosi hicho cha mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa mchezaji huru akitokea West Hama.

Liverpool iliamua kumsajili kipa huyo kutoka West Ham baada ya Simon Mignolet kuondoka kwa mabingwa hao na kujiunga na timu ya Club Brugge.

Hata hivyo, Klopp amewatoa wasiwasi mashabiki wa timu hiyo kuelekea michezo inayofuata huku akidai wataendelea kufanya vizuri kama ilivyo kwa mchezo wao wa kwanza dhidi ya Norwich.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles