25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

LISSU MARUFUKU KUHOJI UHALALI WA JECHA KUFUTA MATOKEO ZANZIBAR

 

NA KULWA MZEE

DAR ES SALAAM

MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amekatazwa kuuliza swali kuhusu uhalali wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salum Jecha kama alikuwa halali kufuta Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar.

Uamuzi wa kumkataza Lissu umetolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alipokuwa akitoa uamuzi kuhusu mabishano yaliyojitokeza yakimtaka shahidi kueleza uhalali wa mwenyekiti huyo kufuta uchaguzi.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni alitakiwa kujibu swali hilo katika kesi ya uchochezi, inayomkabili Lissu na wahariri wa Gazeti la Mawio.

Lissu alipotakiwa kuzungumza kama ana cha kuzungumza, alisema amekubaliana na uamuzi wa mahakama kwa maana haruhusiwi kuuliza kama Jecha Salum Jecha alikuwa na mamlaka ya kufuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar.

Kesi hiyo ya uchochezi inamkabili Lissu, mhariri wa gazeti la MAWIO, Simon Mkina, mwandishi wa habari Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob.Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 8 na 9, mwaka huu,  kwa usikilizwaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles