30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

LISSU KUPELEKWA KUSIKOJULIKANA KWA MATIBABU ZAIDI

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anatarajia kupelekwa ‘kusikojulikana’ kwa awamu ya tatu ya matibabu anayoendelea nayo jijini Nairobi, nchini Kenya.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo hakutaka kuweka wazi nchi anayopelekwa mbunge huyo na kusisitiza kuwa atatolewa nchini Kenya mwisho wa mwezi huu na kupelekwa kusikojulikana.

Pamoja na mambo mengine, Mbowe amesema, Watanzania watarajie kuona picha, video na kusikia sauti ya Lissu na maendeleo yake kwa ujumla.

“Muda mfupi ujao tegeni masikio mtamsikia kwa sauti yake na mtaiona video yake, tunajua bado baadhi yetu wako hatarini na wengine tunaitwa viherehere lakini hatutarudi nyuma, hatutamuogopa yeyote na hatutaukiri umauti.

“Nilikuwa nasita kutoa taarifa za mgonjwa kwa sababu ni haki ya mgonjwa na si jambo la chama, lakini baada ya awamu ya Nairobi lile jukumu ambalo tulijipa la kuwa wasemaji mgonjwa tutawaachia rasmi familia ila hatuwezi kujivua wajibu, tutaendelea kuwajibika nyuma ya familia. Familia ina madaraka makubwa kwa mgonjwa wake kuliko sisi wengine tunaotoa ‘support’,” amesema Mbowe.

Akizungumzia hali ya Lissu, Mbowe amesema jopo la madaktari 12 walipigana kumtibu mbunge huyo nchini Kenya na wakati huo huo hadi kufikia Oktoba 12, mwaka huu gharama za matibabu  ni milioni mia nne na zaidi.

“Sisi kipaumbele chetu hakijawa fedha, ni kumhudumia mgonjwa apone, msitupe kazi ya kuwa msemaji wa Lissu kwenye kila jambo wakati mengine ni ya kifamilia, chama hakijasema kimetoa kiasi gani kwa sababu kila pengo linalopatikana chama kinalipa na asilimia 80 ya michango imetoka kwa Wanachadema,” amesema Mbowe.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles