27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Lissu abwagwa, mahakama yatupilia mbali maombi yake dhidi ya Spika

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amebwagwa mahakamani baada ya maombi yake ya kutaka kufungua kesi kupinga uamuzi wa Spika wa Bunge, Job Ndugai kumvua ubunge wa jimbo hilo kutupiliwa mbali.

Imedaiwa maombi hayo yangesikilizwa hadi mwisho na Lissu kushinda, Jimbo la Singida Mashariki lingekuwa na wabunge wawili ambapo ni kinyume cha Katiba. Pia maombi hayo yemechelewa kuletwa mahakamani.

Akitoa uamuzi huo Jaji Sirilius Matupa leo Jumatatu Septemba 9, amesema maombi ya Lissu hayatekelezeki kwa sababu mleta maombi alitakiwa kufungua kesi ya kupinga uchaguzi mahakamani badala yake wameleta maombi ya kutaka kupinga uamuzi wa spika.

“Mahakama imepata wakati mgumu sana katika kupitia maombi haya kwa sababu kilichotakiwa ni kupinga uchaguzi na lakini hakuna mahali walikofungua kesi mahakamani.

“Tungeruhusu maombi haya hadi mwisho, maana yake Singida Mashariki ingekuwa na wabunge wawili kitu ambacho ni kinyume na Katiba,” amesema Jaji Matupa.

Lissu kupitia Wakili wake Peter Kibatala, aliomba Mahakama Kuu imruhusu kufungua maombi ya Spika kumvua ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles