24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Lingalangala Makamu Mwenyekiti Yanga wa muda 

 Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KAMATI ya utendaji ya klabu ya Yanga, imemteua Thobias Lingalangala kuwa Kaimu Mwenyekiti wa muda hadi hapo uchaguzi utakapofanyika.

Uchaguzi wa Yanga unatarajiwa kufanyika Januari 13, mwaka huu katika nafasi ya Mwenyekiti, Makamu na nafasi nne za wajumbe waliojiuzulu.

Viongozi wa Yanga waliojiuzulu ni Mwenyekiti Yusuph Manji, Makamu  Clement Sanga, wakati wajumbe ni Salum Mkemi, Hashim Abdallah, Omary Saidi na Ayub Nyenzi.

Hivi karibuni viongozi wa Yanga walikutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, kujadili suala la uchaguzi, baadaye Baraza la Michezo la Taifa (BMT), lilitoa uamuzi wa kutaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lisimamie klabu hiyo ifanye uchaguzi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo, alisema Kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga iliyokutana jana ilimteua Lingalangala kuwa Kaimu Mwenyekiti wao hadi hapo uchaguzi utakapofanyika.

“Jana (juzi) kulikuwa na kikao cha Kamati ya utendaji wa Yanga pamoja na TFF, pia kilihudhuriwa na Mwanasheria wetu lakini baadaye walitoka na kuacha Yanga kuendelea peke yao ambao  baadaye walimchagua Lingalangala kuwa kaimu mwenyekiti wa muda hadi hapo watakapofanya uchaguzi,” alisema.

Upande wake Lingalangala, alisema fomu za uchaguzi zilianza kutolewa jana na zitakuwa zikipatikana katika Ofisi za TFF pamoja na makao makuu ya klabu ya Yanga.

“Bei ya fomu kwa upande wa mwenyekiti na kaimu mwenyekiti  itakuwa ni Sh laki mbili, lakini kwa wajumbe itakuwa ni Sh laki moja,” alisema.

Alisema baada ya kikao hicho hakuna kingine kitakachofanyika ila kwa sasa kitakachofuatiwa ni uchaguzi tu.

“Kumekuwa na mambo mengi ambayo yanajitokeza ya kutaka kuchelewesha uchaguzi kutoka kwa baadhi ya wanachama tena wengine wana heshima zao, sasa naomba kwa sasa hali ilipofikia Serikali yetu ipo macho sana kuifuatilia klabu yetu hivyo asitokee mwanachama yeyote atakayetaka kufanya chochote kwani akifanya hivyo mimi nitampeleka moja kwa moja TFF,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles