27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

LHRC yalaani mauaji ya muumini Itigi

Na MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema   kimesikitishwa na tukio la mauaji ya Peter Chambalo.

Chambalo anadaiwa kuuawa na Mkurugenzi wa Wilaya ya  Itigi mkoani Singida ndani ya Kanisa la Sabato.

Taarifa iliyotolewa jana na LHRC na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Paul Mikongoti ilieleza kwamba kitendo hicho  ni uvunjifu wa haki ya kuishi kinyume na ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano 1977 inayoainisha haki ya kuishi kama haki ya msingi ya binadamu.

“Pia ni ukiukwaji wa ibara ya 6 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Raia na Siasa, 1966 unaoainisha haki ya kuishi   na kuweka jukumu la kulinda haki hiyo katika sheria. “kila mtu ana haki ya kuishi”

“Kanuni ya utawala wa sheria inaweka sharti la kutumia utaratibu maalamu kwa mtu yeyote, uliowekwa kisheria katika kutekeleza majukumu bila kujali cheo, hadhi au nasaba ya mtu. Kitendo cha kuingia kanisani kimeingilia uhuru wa kuabudu pamoja na faragha ya kanisa hilo wakati wa kuabudu.

“Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kinalaani na kinakemea tukio hilo lililotweza utu pamoja na kuondoa haki ya kuishi ya mtu huyo.

“Kituo kinalaani tukio hilo kwani lilifanyika kwa ukatili na kutia hofu na taharuki wakazi wa eneo hilo waliokuwa wamekusanyika kwa amani wakifanya ibada siku ya Sabato,” alisema Migongoti katika taarifa hiyo

Alisema LHRC inatoa rai kwa viongozi na watendaji wa Serikali kuzingatia misingi ya Katiba na sheria zilizopo katika kutekeleza majukumu yao.

Kaimu Mkurugenzi huyo alisema wanafutiliwa kwa  karibu tukio hilo na kinatoa wito kwa vyombo vya dola kuendelea kuchunguza na kuwachukulia hatua stahiki wale wote wanatuhumiwa kwa mauaji haya.

Kituo pia kinatoa wito kwa uongozi wa Mkoa wa Singida na Wilaya ya Ikungi kuwahakikishia wananchi wa Itigi usalama wa maisha na mali zao na na kuhakikisha haki ya kuishi inalindwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles