28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

LHRC YAINYOOSHEA KIDOLE NEC UKIUKWAJI WA SHERIA ZA UCHAGUZI

                                                               |Leonard Mang’oha, Dar es Salaam


Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuzingatia misingi ya demokrasia na kutenda haki katika chaguzi mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Julai 23, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga, amesema wameshtushwa na taarifa za kuondolewa kwa wagombea 30 wa vyama vya upinzani katika mchakato wa awali wa uchaguzi mdogo wa madiwani na wabunge unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.

Henga amesema kumekuwapo na hali ya sintofahamu miongoni mwa wananchi katika kata 30 ambazo wananchi wake wamepokwa haki yao ya ushiriki katika uchaguzi huo.

“Wananchi wamepokwa haki yao ya ushiriki katika uchaguzi mdogo baada ya baadhi ya wagombea hususani wa vyama vya upinzani kuenguliwa katika mchakato wa uteuzi wa wagombea kwa sababu mbalimbali zikiwamo tuhuma za kutokidhi vigezo vya kiufundi na kisheria kama kutojua kusoma na kuandika na vigezo vya kutokuwa raia,” amesema Henga.

Amesema kituo hicho kimefuatilia kwa karibu taratibu za awali katika uchaguzi huo wa madiwani uliopangwa kufanyika katika kata 77 sanjari na ubunge katika Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma na kushuhudia matukio mbalimbali yanayoathiri haki za binadamu hususani mchakato wa kidemokrasia unaotaka wananchi kushiriki katika uchaguzi ulio huru na haki kama ilivyoainishwa katika mikataba mbalimbali ya kimataifa, Katiba na sheria za mbalimbali za nchi.

“Kituo kimebaini ukiukwaji wa ibara ya 25 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa wa mwaka 1966, pamoja na Ibara ya tano ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inayoweka haki ya ushiriki wa shughuli za kisiasa kwa kuainisha haki ya kupiga kura,” amesema.

 

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Pongezi kwa LHRC kiukweli hakuna NEC huru imejipa Mabavu kwa Vifungu vya KATIBA ambavyo in KINYUME na HAKI na MISINGI ya Demokrasia, Art.72(12) & Art.41(7) vimeifanya NEC kuharibu system ya UCHAgGUNZI wa HAkI na. kIDEMOKRASIA kwa kujigeuza kuwa Chama Cha Mapinduzi Electoral Commissiqon (CCM-EC)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles