24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

LHRC: UCHOCHEZI UTAFSIRIWE MAHAKAMANI

Na LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM


SIKU moja baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuvipiga faini vituo vitano vya runinga kwa kile kinachodaiwa kukiukwa kwa kanuni za maudhui ya utangazaji, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimetangaza kwenda mahakamani kutafuta tafsiri ya ‘uchochezi’ kisheria.

Pia kituo hicho kimesema kinatarajia kutoa taarifa kwa vyombo vya habari vya kimataifa vinavyohusika na uangalizi wa haki za binadamu, kuomba waingilie kati suala la uhuru wa kujieleza nchini.

Akitoa tamko hilo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk. Helen Kijo-Bisimba, alisema wako tayari kuungana na wadau wengine kwenda mahakamani kuomba tafsiri ya neno uchochezi na baadhi ya vifungu vya kanuni ya maudhui kifungu namba nane.

Mbali na hilo, Dk. Bisimba alisema kuwa wameanzisha harambee ya kuchangia gharama ya kuvisaidia vyombo vya habari vilivyopatiwa adhabu ambayo wao wanaiona kuwa ni uonevu si tu kwa vyombo husika, bali pia kwa uhuru wa kujieleza kwa ujumla.

Novemba 30 mwaka jana, LHRC ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya tathmini ya uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika katika kata 42 katika maeneo mbalimbali nchini.

Kamati ya Maudhi ya TCRA juzi ilivipiga faini vituo vya ITV, EATV, Channel Ten, Azam Two na Star TV vikidaiwa kuwa Desemba 6 mwaka jana viliripoti habari zilizokosa sifa za kimaadili ambazo zingeweza kuhatarisha usalama wa Taifa.

“Tunaitaka Serikali kuheshimu Katiba iliyopo kwa kutokuingilia uhuru wa kujieleza. Ikubali mazuri na mabaya na kuyatumia maoni ya wananchi wake katika kuipatia Tanzania maendeleo endelevu.

“Tunawaomba Watanzania kuungana kuitaka Serikali kutokuchezea uhuru wetu wa kujieleza ambao upo kwa mujibu wa Katiba. Tusiposema sasa tutanyamazishwa kabisa,” alisema Bisimba.

Aidha mkurugenzi huyo alisema kuwa wameiandikia barua TCRA kuitaka kufanya semina kwa LHRC na taasisi nyingine  kuhusu namna bora ya kuandaa maudhui.

“Tunapenda kutoa pole kwa vyombo hivyo na vingine ambavyo vimekumbwa na dhoruba ya adhabu kutoka kwa Serikali, hasa kwa kutoa taarifa zisizoifurahisha,” alisema…….

Kwa habari zaidi, jipatie nakala yako ya MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles