KYLIE JENNER, TRAVIS SCOTT NDOA YAKARIBIA

0
752

NEW YORK, MAREKANI


STAA wa mitindo kutoka familia ya Kardashian, Kylie Jenner na baba wa mtoto wake, Travis Scott, wameanza kufikiria juu ya kufunga ndoa.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye ametajwa kuwa miongoni mwa matajiri wenye umri mdogo, alifanikiwa kupata mtoto na rapa huyo mwenye umri wa miaka 26 miezi sita iliyopita na kumpa jina la Stormi.

Kila siku zinavyozidi kwenda, wawili hao wamekuwa wakioneshana mapenzi zaidi, lakini wameweka wazi kwamba, japokuwa wanapanga kufunga ndoa, lakini hawana haraka sana ila mipango bado inaendelea.

Inasemekana kuwa mama wa familia ya Kardashian, Kris Jenner, amekuwa na ushawishi mkubwa kwa wawili hao kufikia mipango ya kutaka kufunga ndoa, akidai kuwa mastaa hao wanapendezana tofauti na uhusiano wa kwanza wa Kylie na rapa Tyga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here