KWAYA YA AICT CHANG’OMBE KUADHIMISHA MIAKA 30

0
281

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kwaya ya Kanisa la African Inland Church (AICT) Chang’ombe maarufu CVC ya jijini Dar es salaam inatarajia kufanya maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwake.

Katibu Mtendaji wa CVC, Hosea Kashimba amesema, tukio hilo litakutanisha kwaya zote maarufu zikiwamo, Kinondoni Revival, Tumaini Shanilieni ya Arusha, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Uinjilisti Kijitonyama, KKKT Msasani na nyingine nyingi.

“Maadhimisho hayo yataanza Aprili 28, mwaka huu kwa kuweka jiwe la msingi wa Kituo cha Mikutano cha kwaya hiyo eneo la Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam,” amesema Kashimba.

Pamoja na mambo mengine, Kashimba amesema katika tukio la kuweka jiwe la msingi la kituo hicho linatarajiwa kuwekwa na Askofu wa Kanisa hilo Dayosisi ya Pwani, Charles Salalah.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here