26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kujenga nyumba za tetemeko Kagera ni Sh bilioni 880

tetemeko1

Na EDITHA KARLO,

SERIKALI mkoani Kagera imesema  tathimini iliyofanyika  ya athari za tetemeko la ardhi mkoani hapo imebaini ujenzi wa makazi ya watu kurejea kwenye hali yake kunahitaji   Sh bilioni 880  huku ujenzi wa miundombinu  ya serikali ukihitaji Sh bilioni  tisa.

Mkuu wa Mkoa Kagera, Meja Jenerali (mstaafu), Salum Kijuu, aliyasema wakati akipokea msaada wa fedha  na vitu mbalimbali yakiwamo  mablanketi  na vyandarua kutoka kwa taasisi ya Adra Tanzania ya Kanisa  la Adventisti Tanzania lenye makao makuu yake   Arusha.

Kijuu alisema hadi sasa fedha zilizoingizwa katika akaunti ya maafa ya Kagera ni   Sh bilioni nne  ambazo hazitoshelezi katika ujenzi wa makazi ya watu.

Alisema   serikali  imependekeza  vifaa vingine vipelekwe katika taasisi za umma vikiwamo vituo vya afya na  shule  wananchi waendelee kupata huduma kama ilivyokuwa  awali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles